OFISI YA TAKWIMU NA WAKALA WA REA WAANZA SENSA KUJUA WATUMIAJI WA UMEME,SOMA HAPO KUJUA
Mwakilishi
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw.Ephraim Kwesigabo akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari juu ya utafiti watakaoufanya kwa pamoja na Wakala wa
Nishati Vijijini(REA) ukiwa na lengo la kukusanya takwimu rasmi zinazohusu hali
ya upatikanaji wa nishati ya umeme katika maeneo ya vijijini.Kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga
|
KATIKA
kuhakikisha wanajua idadi hasa ya wananchi wanaotumia nisharti ya umeme nchini,Serikali
imeanza utafiti wa kuangalia hali ya upatikanaji wa Nishati hiyo katika mikoa 26 ya Tanzania bara
wa mwaka 2016 kuanzia Octoba 10, hadi Novemba 15 mwaka huu.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Ephraim Kwesigabo
amesema kuwa utafiti huo unafanya na Serikali kupitia Wakala wa Nishati
Vijijini(REA) kwa kushirikiana na kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS).
Dkt
Kwesibago amesema kuwa lengo la utafiti huo ni kukusanya takwimu rasmi
zinazohusu hali ya upatikanaji wa Nishati umeme katika ngazi ya jumuiya na kaya
ili kujua matumizi ya umeme na nishati pamoja na faida zake kwa maendeleo.
Sambamba
na ukusunyaji wa takwimu hizo, Dkt Kwesibago amesema kuwa utafiti huo
utahusisha ukusanyaji wa takwimu za kidemografia na za kiuchumi za wanakaya
zikijumuisha umri, jinsia, hali za ndoa, elimu, shughuli za kiuchumi, matumizi
ya muda pamoja na ushiriki wa jinsia katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
Ameongeza
kuwa utafiti huo utahusisha jumla ya maeneo 676 ya vijiji na mijini
yaliyochaguliwa kitaalam katika mikoa yote ya Tanzania bara na kuhusisha jumla
ya kaya binafsi 10,140 pamoja na viongozi wa vijiji na mitaa 676 ambao
watahojiwa kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopatikana katika maeneo
yao.
Aidha,
amesema kuwa timu ya wadadisi wapatao 130 watahusika katika zoezi hilo la
ukusanyaji taarifa ambapo kila mkoa utakuwa na wadadisi watano, msimamizi mmoja
na wataalamu wengine kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu makao makuu.
Vile
vile alisema kuwa upatikanaji wa takwimu hizo utasaidia katika kuandaa taarifa
kuhusu hali halisi ya upatikanaji na usambazaji wa nishati ya umeme nchini na
hivyo kuweza kupima na kuhakiki maendeleo yaliyofanikiwa na mafanikio ya juhudi
za Serikali.
Pia
taarifa za utafiti huo zitatumika katika kuendeleza mipango ya usambazaji
wa umeme vijijini kupitia miradi mbalimbali itakayotekelezwa na Serikali kwa
ajili ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati bora vijijini.
Mbali
na hayo wananchi wameombwa kutochukua sheria mkononi kwa kuwadguru wadadisi
wanapokuwa wakifanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya kusaidia nchi yetu kupata
takwimu rasmi zinazosaidia katika kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo.