RAIS MAGUFULI AGOMA TENA KWENDA ULAYA,SASA AAMUA KUMTUMA PROFESA TIBAIJUKA,SOMA HAPO KUJUA
Rais Dk. John Magufuli, amemteua aliyekuwa
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
kumwakilisha katika mkutano wa makazi wa Habitat III unaofanyika katika mji wa
Quito, Ecuador.
Taarifa iliyoituma kwenye mitandao ya jamii na
Profesa Tibaijuka jana, ilisema katika msafara huo amefuatana na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Mandeleo ya Makazi, Dk. Yamungu
Kayandabila.
“Hivi sasa niko Geneva, Uswisi kwa
matayarisho nikielekea Quito Ecuador mkutano wa makazi duniani wa HABITAT
III kumwakilisha Rais wetu nikiwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya
Ardhi,namshukuru Rais kwa heshima hii kubwa, Sitamuangusha.
Habitat III,ni mkutano wa uamuzi na
mustakabali wa Shirika la Makazi Duniani na agenda ya maendeleo endelevu ya
miji.
“Kama tunavyojua mkutano wa Habita I
ulifanyika Vancouver,Canada mwaka 1976, Habitat II ulifanyika Istanbul, Uturuki
mwaka 1996 na huu Ecuador Marekani ya Kusini 2016,”alisema.
Alisema kila baada ya miaka 20 wakuu wa nchi
hukutana kukubaliana namna ya kuendeleza makazi kupitia Shirika la UNHABITAT
ambalo aliwahi kuliongoza kwa miaka 10.
“Rais Magufuli alichaguliwa na kuongoza
Baraza la Uongozi wa shirika hilo (Governing Council) kwa muhula wa mwaka
2006/2008 alipokuwa Waziri wa Ardhi.
“Wafanyakazi walimpenda kiasi kwamba
alipobadilishwa wizara na kupelekwa Mifugo na Uvuvi karibu iwe zogo
ofisini kwangu wakidai tutayumba.
“Niliwatuliza na kuwaambia kumbadilisha
wizara hakumuondolei uenyekiti wake na kweli aliendelea nao na kumaliza,”alisema
Tibaijuka.
Alisema katika mkutano huo, jambo kubwa
atakalolipigania ni utaratibu wa shirika hilo kuzisaidia nchi zinazoendelea
kama sisi kwa kuzikopesha halmashauri zao fedha za miundombinu, bila
kuilazimisha Serikali kuu kutoa dhamana kwa mikopo hiyo.
Alisema jambo hilo ni la msingi kwa
vile huleta kasi ya maendeleo ingawa huwa linapingwa na wakubwa
wanaotaka kukopa kupitia Serikali kuu ili waibane kwa kutumia Benki
ya Dunia, kitendo ambacho kinachelewesha kasi ya maendeleo.
“Tutajitahidi kulingana na maelekezo ya Rais
tunayemwakilisha kuhusu msimamo wa nchi yetu na washirika wake ambao ni nchi za
Afrika na za G77 na China,” alisema.