SERIKALI YAMZUIA MAMA LWAKATARE,SOMA HAPO KUJUA
Serikali imesitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa
na Mchungaji Getrude Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko magerezani
hadi hapo utaratibu mwingine utakapotolewa.
Mpango huo unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana
na Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha
wafungwa 78 kutoka magerezani baada ya kuwalipia faini inayofikia Sh25
milioni.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi
alisema amepata maelekezo ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka ngazi ya juu ya
jeshi hilo.
Alisema wananchi wengine bado wanaweza kuwalipia
faini hiyo ndugu zao. Mrema alisema jana kuwa mpango huo ulilenga kupunguza
msongamano magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa.