Zinazobamba

CCM YAJIVUNIA USHINDI WA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA,VITONGOJI NA VIJIJI


Na Mussa Augustine.

Chama cha Mapinduzi (CCM)kimebainisha kuwa ushindi uliyopatika kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vitongoji na Vijiji inaonesha kua ni imani ya watanzania kwa chama hicho nakwamba kitaendelea kuwatumikia vyema katika kuwaletea Maendeleo. 

 Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 29,2024 na Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo Taifa wa Chama hicho CPA Amos Makalla wakati akizungumza na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika Ofisi ndogo za chama hicho Lumumba Jijini Dar es salaam. 

 CPA Makalla amesema kuwa ushindi huo umeleta tafsiri kuwa wananchi bado wana imani na chama hicho nakwamba kwa sasa kilichobaki ni kuchapa kazi ili kuleta Maendeleo kwa Wananchi. 

 "Nawashukiru watanzania kwa kukipa kura za ushindi chama Cha Mapinduzi,pia nawaomba wale wote walioshinda katika uchaguzi huo kuanzia ngazi za Mitaa,Vitongoji na Vijiji, kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha wanatekeleza vyema ilani ya CCM"amesema CPA Makalla 

 Nakuongeza kuwa "wale waliioshinda waliomba utumishi kwa wananchi,na wananchi wakawachagua, hivyo sasa tunataka wawajibike kwa wananchi,pia kufanya vikao vya mapato na matumizi kwa wananchi kama ilani yetu inavyoelekeza. 

 CPA Makalla amesema mafanikio yaliyopatikana katika uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoiongoza ndiyo iliyochangia kupata ushindi huo kwa kishindo kwani wagombea wote walifanyiwa tathmini na chama na kisha wakapitishwa na chama hicho hali iliyopelekea ushindi mnono. 

 Kuhusu migogoro ndani ya vyama vya siasa Makalla amesema migogoro hiyo ya vyama vya upinzani pia imesababisha CCM kushinda kutokana na wananchi kukosa Imani na vyama hivyo.

 "Nyie mlishuhudia migogoro ikiwemo baina ya viongozi wao huyu akimtuhumu yule hivi na yule akimtuhumu huyu hivi na wengine wanatuhumiana kwa kukaa katika uongozi muda mrefu bila kumpisha mwenzake na siku zote hamuwezi kushinda kama una migogoro wapatane Sasa huko" amesema. 

 Amesema pamoja na ushindi huo pia Kuna vijiji ambavyo walikuwa katika uongozi kwa muda mrefu lakini kupitia uchaguzi huu baadhi yake vimeenda kwa upinzania na wao kama chama wanakubali kwani ndiyo demokrasia. 


 Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya matokeo ya uchaguzi huo yaliyotangazwa jana Novemba 28,2024 na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais,TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amesmea kuwa katika nafasi ya uenyekiti wa kijiji chama cha Mapinduzi (CCM) kimeongoza kwa asilimia 99.01 kikifuatiwa na Chadema. Kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji ni 12,271 kati ya nafasi 12,280 zilizopaswa kufanya uchaguzi. 

Kati ya nafasi hizo, CCM imeshinda nafasi 12,150 sawa asilimia 99.01,Chadema imeshinda nafasi 97 sawa na asilimia 0.79,ACT Wazalendo imeshinda nafasi 11 sawa na asilimia 0.09,CUF imeshinda nafasi 10 sawa na asilimia 0.08 NCCR Mageuzi imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia.0.01, UMD imeshinda nafasi 1 sawa na.asilimia 0.01,na ADC imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia.0.01.

Hakuna maoni