SAMIA SULUHU AMSHAMBULIA KIKWETE WAZI WAZI,SOMA HAPO KUJUA
SAMIA Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ‘ameikandia’ Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya
Kikwete na kusema imeacha mzigo mkubwa wa madeni, anaandika Dany Tibason.
Samia
amesema kutokana na mzigo mkubwa wa madeni ambao wameirithi kutoka katika
serikali ya awamu ya nne, licha ya serikali kukusanya Sh. 1.3 trilioni kwa
mwezi lakini madeni yanayolipwa kila mwezi ni Shilingi bilioni 900.
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akifungua mkutano wa
waganga wakuu wa mikoa, halmashauri na waganga wafawidhi wa hospitali za mikoa
na kanda mbalimbali hapa nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo
cha Mipango mjini Dodoma.
“Huu siyo wakati wa kutegemea kila kitu kutoka serikalini,
kusema ukweli kwa bahati mbaya tulipoingia madarakani tulikuta madeni makubwa
ambayo yaliachwa na serikali ya awamu ya nne, lazima tulipe madeni hayo,”
amesema.
Bila kutoa ufafanuzi wa madeni hayo kama ni ya ndani
au nje ya nchi Mama Samia amesema serikali ya awamu ya tano ilikutana na mzigo
mkubwa wa madeni ambao haukwepeki kwani serikali inapoingia madarakani hurithi
madeni na mali za serikali iliyomaliza muda wake.
Amezitaka hospitali za serikali kote nchini kuepuka
migogoro katika sekta ya afya kwa kufunga mitambo ya kielekroniki kwa ajili ya
kukusanya mapato ambayo yatawezesha ulipiaji wa mahitaji mbalimbali ikiwa ni
pamoja na ununuzi wa madawa.
“Serikali bado inajipanga kuona ni jinsi gani ya
kuwezesha katika sekta muhimu na ndiyo maana serikali ya awamu ya tano imeweza
kupitisha bajeti kubwa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto tofauti na miaka yote tangu nchi ipate Uhuru,” amesema Samia.