FREEMAN MBOWE AKWAA KISIKI MAHAKAMANI,KESI YA JENGO LA NHC YAMTOA NISHAI,SOMA HAPO KUJUA
Mahakama kuu kitengo cha Ardhi imetupilia mbali kesi
ya maombi ya kurejea katika jengo iliyokuwa ofisi ya Tanzania Daima pamoja na
ukumbi wa bilcanas.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji mfawidhi wa
mahakama hiyo, Sivangilwa Mwangezi ambaye amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa
kuondoa vitu katika jengo hilo.
Amesema katika hukumu hiyo hakuna mtu aliyevunjiwa
haki yake ya msingi kutokana na kufuatwa kwa Sheria dhidi ya madai ya Shirika
la Nyumba NHC, kwa Mbowe HotelS.
Wakili wa upande wa NHC, Aliko Mwamnenge amesema
kutokana na hukumu hiyo Mbowe hotelS wanadaiwa sh. Bilioni 1.7 na NHC.Amesema
vitu haviwezi kurudishwa mpaka pale mlalamikiwa atakapolipa deni lake kwa NHC.
Nae Wakili upande Mbowe Hotel, John Malya amesema
wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi.Amesema kuwa nakala
wakiipata wanaweza kuamua katika kukata rufaa.