MABARAZA YA ARDHI YALIA NA UHABA WAWATUMISHI,SOMA HAPO KUJUA
MABARAZA ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na
Mikoa yanakabiliwa na upungufu wa watumishi na vifaa hali
inayopelekea mashauri kutokusikilizwa kwa wakati.
Imeelezwa kuwa Mabaraza hayao yana kesi za wananchi 14,163 nchi nzima
ambapo kila baraza linamwenyekiti mmoja ambapo wanashindwa kufanya kazi kwa
ufanisi kama inavyotakiwa.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam leo
na Kaimu Msajili Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya,
Amina Rashidi.
“Manispaa ya Kinondoni inakesi paka sasa 2385 na
mwenyekiti mmoja ambapo tumejiwekea kwa mwezi mwenyekiti mmoja anatakiwa
kusikiliza kesi 30 hadi 40, tunalazimika kuchukua watendaji wengine Ilala na
Temeke ili wasaidiane” amesema Bi Rashidi
Amesema kasi ndogo ya uundaji wa Mabaraza ya Ardhi
na Nyumba ya Wilaya imesababisha wananchi kulazimika kufuata mbali
huduma za utatuzi wa migogoro.
“Tunahitaji wafanyakazi 411 lakini paka sasa
tunawafanyakazi 179 tu katkika mabaraza 53, tunaiomba serekali itusaidie kupata
watendaji hao” amesema Bi Rashidi.
Amina amesema mazingira yasiyoridhisha ambayo ni
pamojana na ukosefu wa ofisi, maktaba kwa ajili ya rejea za sheria mbalimbali
na ukosefu wa samani na vitendea kazi nayo yamechangia mashauri
yasikilizwe kwa wakati.
“Mbali na matatizo hayo pia mabaraza hayo yamekuwa
yakikabiliwa na matatizo ya kuchelewa kufanyika kwa ukaguzi wa maeneo na
migogoro kutokana na ukosefu wa usafiri ,”alisema Amina.
Amina alisema ili mashauri yaweze kusikilizwa na
kuamuliwa katika muda mfupi , serikali inatakiwa kuimarisha Mabaraza ya
Ardhi na Nyumba ya Wilaya yaliopo kwa kuhakikisha inatatua matatizo
yanayokabili mabaraza hayo na pia kuweka mfumo wa kielektroniki kwa ajili
ya kutunza kumbukumbu.
“ Mabaraza hayo yanawajibu mkubwa wa
kuwaondolea wananchi kero ya migogoro ya ardhi na nyumba kwa
haraka na kwa gharama nafuu ,hivyo serikali inatakiwa kuwajibika kwa
weananchi kwa kuhakikisha kuwa mabaraza yaliopo yanaimarishwa,kasi ya kuunda
Mabaraza mapya inaongezwa na yanawezeshwa,”alisema. Amina.