MAAMUZI YA TTF KWENYE KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA,SOMA HAPO KUJUA
Kamati
ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imeipiga faini ya sh.
5,000,000 (milioni tano) klabu ya Simba, kuiagiza ilipe gharama za uharibifu wa
viti uliofanywa na washabiki wake katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya
timu yake na Yanga iliyochezwa Oktoba Mosi mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Pia
Kamati hiyo katika kikao chake kilichofanyika jana (Oktoba 4, 2016), imelaani
kitendo hicho na kuionya klabu hiyo kuwa vitendo vya aina hiyo vikiendelea
itakabiliwa na adhabu kali zaidi ikiwemo kucheza mechi bila washabiki. Adhabu
dhidi ya Simba imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 42(3) na 24(7) za Ligi Kuu.
Vilevile
kwa kuzingatia Kanuni ya 9(8) ya Ligi Kuu, Kamati imefuta adhabu ya kadi
nyekundu iliyotolewa na mwamuzi wa mechi hiyo kwa Jonas Mkude wa timu ya Simba
baada ya kuthibitika bila mashaka kuwa nahodha huyo hakustahili kadi hiyo.
Mbali
ya ripoti ya Kamishna na kupitia tena mkanda wa mechi hiyo iliyoonyeshwa
‘live’, Kamati inaendelea na uchunguzi wa jambo lingine kuhusu uchezeshaji wa
mwamuzi wa mechi hiyo Martin Saanya, na wasaidizi wake Samwel Mpenzu na
Ferdinand Chacha kabla ya kutangaza uamuzi wake.
Mkuu
wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amepigwa faini ya sh.
200,000 (laki mbili) kwa kuingia uwanjani baada ya mechi hiyo wakati yeye
hakuwa miongoni mwa maofisa wa mechi waliotakiwa kuwepo katika eneo hilo.
Adhabu
dhidi ya Manara ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(10). Eneo husika ni kwa ajili ya
wachezaji, mabenchi ya ufundi, waamuzi, madaktari, huduma ya kwanza, wapiga
picha na maofisa wengine wa mechi.
Klabu
ya Azam imepigwa faini ya sh. 3,000,000 (milioni tatu) kwa kuvaa nembo ya
mdhamini wa Ligi Kuu kwenye mkono mmoja tu badala ya miwili ambapo ni kinyume
na Kanuni ya 13(1), na adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 13(6).
JKT
Ruvu imepewa onyo na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya
Msimamizi wa Kituo, na Ofisa wa Bodi ya Ligi kushambuliwa na mshabiki wa timu
hiyo katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyofanyika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi
mkoani Pwani. Mshabiki huyo amefungiwa miezi 12, na iwapo vitendo hicho
vitaendelea Uwanja huo utafungiwa kwa mechi za Ligi Kuu.
Mwamuzi
Ahmed Seif amefungiwa miezi sita kwa kushindwa kumudu mechi kati ya African
Lyon na Mbao FC ikiwemo kutoa adhabu ya penalti ambayo haikuwa sahihi. Pia
Mwamuzi huyo alipata alama za chini ambazo hazimruhusu kuendelea kuchezesha
mechi za Ligi Kuu ya Vodacom.
Pia
Makamisha David Lugenge na Godbless Kimaro wamepewa onyo kwa kuwasilisha
taarifa zenye upungufu katika mechi walizosimamia za raundi ya tano na saba.
Katika
Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Mbeya Warriors imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki
mbili) kwa kupitia mlango usio sahihi ikiwemo kuvunja kufuli kwenye mechi kati
yao na Kimondo FC iliyofanyika Septemba 24 mwaka huu Uwanja Vwawa mkoani
Songwe. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Daraja la Kwanza