KUKURUPUKA KUMPONZA MKURUGENZI WA MAGUFULI,CHAMA CHA WALIMU WAAPA KUFA NAYE MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA
CHAMA cha Walimu (CWT) na Umoja wa Wakuu wa Shule za
Msingi katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wamesema kuwa, wapo katika
hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kisheria ili kumfikisha mahakamani
Kiomoni Kibamba, mkurugenzi wa jiji hilo, anaandika Moses Mseti.
Ni kutokana na kumpinga hatua
ya Kibamba kuwasisimamisha na kuwavua madaraka wakuu wa Shule za Msingi 62 kwa
madai kwamba, walisajili wanafunzi hewa katika shule zao kwa lengo la kujipatia
fedha.
Msimamo huo umetolewa leo na Asha Juma, Katibu wa
Umoja wa Wakuu wa Shule Wilaya ya Nyamagana mbele ya waandishi wa habari na
wakuu wa shule hizo waliosimamishwa na kuvuliwa madaraka.
Asha amesema kuwa, mkurugenzi wa jiji hilo alichukua
uamzi wa kukurupuka huku akidai, hana mamlaka ya kumfukuza mwalimu yeyote.
Hata hivyo amesema, wapo katika hatua za mwisho za
kukamilisha taratibu na kwamba muda wowote kuanzia sasa watamfikisha kortini
ili kujibu tuhama za kuwafukuza walimu hao bila kufuata taratibu.
“Kama sio maamzi ya kukurupuka ni kitu gani, haiwezekani.
Kuna walimu wametangulia mbele za haki na wengine sasa hivi wameteuliwa kuwa
viongozi ngazi tofauti serikalini lakini na wao wamejumuishwa humo.
“Kuna mwalimu January Sigareti ameteuliwa kuwa DC
(Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Tanga), Abas Mohamed (amestaafu), Nasoro Rashid
(amefariki) na Jummane Nyanda ambaye alipata ofa kuwa Ofisa Elimu Vifaa na
Takwimu Buhingwe, Geita na wao wamo, kama sio kukurupuka ni nini?” amehoji.
Amesema kuwa, mkurugenzi huyo alishindwa kufanya
uchunguzi wa kina na kuanza kuchukua hatua ikiwemo kitendo cha kuorodhesha
walimu waliofariki muda mrefu kwamba wapo katika vituo vyao vya kazi.
Hata hivyo mkurugenzi Kibamba alipotafutwa na
mtandao huu kuzungumzia suala hilo, alidai hawezi kutengua uamzi wake na
kwamba, vyombo vyake vilifanya uchunguzi na kupata ukweli wa walimu kusajili
wanafunzi hao