KESI ZA UCHOCHEZI ZASHAMILI MAHAKAMANI,TUNDU LISSU ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI NA KUIBUKIA MWANZA,SOMA HAPO KUJUA

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, jana
alishindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kujibu mashitaka
ya uchochezi huku mdhamini wake akiieleza mahakama kuwa, yupo jijini Mwanza
akisimamia kesi ya Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda katika Mahakama Kuu ya
Mwanza.
Lissu ambaye pia ni wakili wa Mahakama Kuu na
mwansheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo anashitakiwa kwa uchochezi
pamoja na washitakiwa wengine ambao ni ni Jabir Idrissa, mwandishi mwandamizi
wa Gazeti la MAWIO, Simon Mkina, mhariri wa Gazeti hilo na Ismail Mehboob,
meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti ya Flint
.
Mdhamini wa Lissu, Ibrahim Hemed, alitoa taarifa ya
kutofika kwa mdhamana wake mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas
Simba.
Ibrahim alidai kwamba Lissu amempatia taarifa kuwa
ameshindwa kufika kwa sababu yupo kwenye kesi ya uchaguzi huku Peter Kibatala
wakili wa utetezi akiiomba mahakama ipokee taarifa za Lissu na ikubali
kuhairisha kesi hiyo.
“Lissu ni wakili pekee wa
mlalamikiwa Esther Bulaya katika kesi ya uchaguzi,” alisema
Kibatala.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba
aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 31 mwaka huu.
Katika kesi hiyo Lissu anaunganishwa kama mshitakiwa
kufuatia kunukuliwa akitoa maoni yake katika habari iliyochapishwa na gazeti la
MAWIO ikiwa na kichwa cha habari “Machafuko yaja Zanzibar.