Zinazobamba

KUBWA ZAIDI WIKI HII DAR ES SALAAM-NI MAANDAMANO YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MJUKUU WA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W),SOMA HAPO KUJUA



Pichani ni Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum wa pili kutoka Kushoto akiwa katika matembezi maalum yaliyofanyika Jijini Dar es salaam yaliyoandaliwa na waumini wa Shia Ithanasheriya Tanzania ikiwa ni Ishara ya kumkumbuka Mjukuu wa mtume Muhamad ambaye ni Imam Hussein.

Kiongozi mkuu wa waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akizungumza na wanahabari wakati wa maandamano hayo Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine Sheikh Jalala amendelea kusisitiza watanzania kutunza  amani na umoja uliopo pamoja na kufwata yale ambayo Imam Hussein alikuwa akiyafwata wakati wake ikiwemo kupinga ukandamizwaji,dhuluma katika jamii na kujenga umoja na mshikamano katika jamii.


Waumini wa Dini ya kiislam Kutoka jumuiya ya kiislam Khoja Shia Ithnasheriya Tanzania wakiwa katika maandamano ya amani Jijini Dar es salaam  ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w),ambaye ni Imam Hussein (a.s),maandamano ambayo yameanzia katika msikiti wa Kablastan posta Jijini Dar es saalaam hadi katika msikiti wa Khoja Shia Ithnasheriya Tanzania uliopo posta.PICHA ZAIDI ZINAENDELEA

 




















RAI imetolewa kwa Waislam nchini kujitoa kwa moyo wote katika kupambana na mambo yasiyo faa katika jamii ili kuweza kujiweka katika mipango mizuri ya kutokemeza  matendo maovu katika jamii.Anaandika Karoli Vinsent,endelea nayo.

Akizungumza na wanahabari wakati wa maandamano katika  Matembezi maalum yaliyofanyika Jijini Dar es salaam wiki hii ambayo  yaliyoandaliwa na waumini wa Shia Ithanasheriya Tanzania ikiwa ni Ishara ya kumkumbuka Mjukuu wa mtume Muhamad ambaye ni Imam Hussein,

Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum alitumia nafasi hiyo kuwataka waislam kufuata Nyayo za Iman Hussein ambaye alipenda haki na kukataaa dhuluma miongoni mwa Jamii pamoja na kutunza amani ilipo nchini Mwetu.

Hata hivyo Sheikh huyo amezitaka Taasisi za kidini nchini kujenga Umoja na mshikamano miongoni mwao bila kujali imani na itikadi za dini zao ili kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano na upendo kwa wote.