Zinazobamba

KIJANA ALIYETOBOLEWA MACHO NA SCORPION,MADAKTARI WATOA JIBU HILI,SOMA HAPO KUJUA

 

makonda-said-macho-11

Ukiachana na Tukio la Walimu kumuadhibu kikatili mwanafunzi Sebastian Chinguku wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya, tukio lingine ambalo limeendelea kutikisa vyombo vya habari ni kuhusu kijana Saidi Ally anaedaiwa kutobolewa macho na kijana maarufu kwa jina la ‘Scorpion’.makonda-said-macho-1

Kufuatia jitihada za serikali na kupelekea kukamatwa kwa kijana huyo anaedaiwa kufanya hivyo na kufikisha mahakamani licha ya kukana kilichotokea, Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam chini Mkuu wa Mkoa Paul Makonda imehaidi kuendelea kumsaidia kijana huyo baada ya jitihada za kumponya kugonga mwamba na taarifa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kueleza kuwa aliyemtoboa macho kijana huyo aliharibu baadhi ya mishipa inayompelekea mtu kuona.makonda-said-macho-7

Hivyo Serikali ya Mkoa imeahidi kumuwekea Macho ya bandia, kumsomesha, kumpatia fimbo maalum ya walemavu wa macho, atapatiwa wataalamu maalum kwa ajili ya kumfundisha ili hayazoee mazingira, atapewa dereva maalum ambaye atakuwa anampeleka sehemu mbalimbali ikiwemo hospitali kwa ajili ya huduma tofauti, pia serikali itampatia kiasi cha shilingi milioni 10 ili awekeze kwenye biashara yake ya saluni, na serikali itaandaa kampeni maalum ili aweze kuchangiwa na watanzania wenzake.

Kwa upande wake kijana huyo aliyetobolewa macho Saidi Ally ameeleza kuwa anamshukuru Mkuu wa Mkoa Paul Makonda na Rais Magufuli kwa kuendelea kumuunga mkono, na kueleza masikitiko yake kwakutoweza kuona tena, huku akiiomba serikali impatie malazi kwanai ni kitu ambacho kinadumu milele.makonda-said-macho-8

Jiunge nasi