WAZIRI MKUU AWANGUKIA WAFANYABIASHARA NA MABALOZI,NI KUHUSU TETEMEKO LA ARDHI,SOMA HAPO KUJUA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongea na Mabalozi na
Wawakilishi wa wafanyabishara Ikulu jijini Dar es Salaam kutoa taarifa ya
tatemeko la ardhi na maafa yaliyotokana tarehe 10 September 2016.
Waziri Majaliwa amewaomba wawakilishi hao kutoa
misaada mbalimbali ili kuungana na Serikali kuwasaidia walioathirika mkoani
Kagera.
Baadhi ya Taasisi na Balozi zilizo ahidi
kutoa michango ni:-
Ubalozi wa China – Milioni 100
Ubalozi wa Kuwait – Euro 10,000
Ubalozi wa Kenya- wametoa mabati na malazi
Kampuni ya China Mercharnt Group – Mil 100
Mo Dewji – Milioni 100
Toyota Ltd – Milioni 10
TBL – Milioni 100
Woolworth -Milioni 20
Sahara Tanzania – Milioni 20
Azania Group – Milioni 20
Kagera Sugar -Milioni 100 na Tani 10 za sukari
Nosime Group- Milioni 75
Tanga Cement – Mifuko 1000 ya Saruji
Reginald Mengi – Milioni 110
Protas Ishengoma- Wakili na mhanga wa tetemeko
Milioni 5
GBP, MOIL,&OILCOM- Watajenga shule mbili
zilizoharibika
Vile vile Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
ametangaza matembezi ya kukumbuka janga hilo na kuahidi wananchi wote na
mashirika mbalimbali kujitokeza katika matembezi hayo yatakayo fanyika siku ya
Jumamosi asubuhi katika maeneo ya Masaki.
Taarifa zaidi za Matembezi haya zitatolewa katika
vyombo vya habari.