FREEMAN MBOWE AONYESHA UPENDO WAKE KWA WALIPATA MAJANGA TETEMEKO LA ARDHI,YUMO PIA RAIS KENYATA,SOMA HAPO KUJUA
Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta amezungumza
kwa njia ya simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe
Magufuli kumpa pole kufuatia vifo vya watu na madhara mengine yaliyotokana na
tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Tetemeko lililotokea mkoani Kagera Septemba 10,
limesababisha vifo vya watu 16, kuacha watu 253 wakiwa na majeraha mbalimbali
ya mwili na nyumba zaidi ya 1000 zikiwa zimebomolewa.
Taarifa kutoka kwa msemaji wa Rais Kenyatta alisema
kuwa Rais Kenyatta ameahidi kutoa msaada wa mabati, blanketi na magodoro ili
kuwasaidia watu wasio na makazi mkoani Kagera.
Msaada huo utasafirishwa kwa ndege na Jeshi la Kenya
Jumanne hii Septemba 13 hadi mkoani Kagera ambapo ndipo palipopata
madhara.
Katika hatua nyingine,
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, jana aliwasili mjini Bukoba kuwatembelea
waathirika na kutoa mkono wa pole kwa kaya 16 za waliofikwa na misiba kutokana
na tetemeko hilo la ardhi.
Mbowe alitoa shilingi milioni 2.1 kwa ajili ya kaya
hizo, mifuko 150 ya sementi kwa familia 15 ambazo zimepoteza makazi ambapo kila
kaya ilipata mifuko 10.
Mwenyekiti huyo wa Chadema aliambatana na viongozi
wengine wa Chadema mjini humo pamoja na Mbunge wa Bukoba Mjini, Willfredy
Rwakatale na Mbunge wa viti maalum (CUF), Saverina Mwijage, walitoa sukari
sukari kilo 25 pamoja na mchele kilo 50.
“Ndugu zangu, tukio hili sio la Serikali
au chama chochote, ni jambo la kitaifa. Serikali inapaswa kutenga fungu kubwa
kwa ajili ya kuisaidia jamii,” Mbowe
anakaririwa.
Akiwa katika shule ya Sekondari ya Ihungo
iliyobomolewa na tetemeko la ardhi na kusababisha wanafunzi kukosa madarasa ya
kusomea, Mbowe ambaye pia alisoma katika shule hiyo alitoa misaada mbalimbali.
Rais John Magufuli alilazimika kuahirisha safari
yake ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais wa Zambia, Edgar Lungu kutokana na janga
la tetemeko la ardhi, badala yake alimtuma Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan
kumuwakilisha