SERIKALI YAENDELEA NA SINEMA KWENYE AJIRA ZA WALIMU,LEO WAIBUKA NA HILI,SOMA HAPO KUJUA
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma
Serikali imeanza kupanga walimu wa sayansi moja kwa
moja katika shule badala ya Halmashauri kama ilivyokuwa awali ili kuleta uwiano
sawa wa walimu katika shule mbalimbali nchini.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais (TAMISEMI) Suleman Jaffo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Muleba Prof.
Anna Tibaijuka lililohusu mkakati wa Serikali katika kukabiliana na tatizo la
upungufu wa walimu.
Naibu Waziri Jaffo amesema kuwa Serikali
imeandaa mkakati wa kuwaajiri wahitimu wa shahada za sayansi ambazo siyo za
ualimu baada ya kuwapa mafunzo ya muda mfupi kuhusu mbinu za ufundishaji na
maadili ya ualimu ili kukabiliana na changamoto ya walimu wa sayansi nchini.
Naibu Waziri Jaffo amesema kuwa tayari kibali
kimeombwa katika Ofisi ya Rais Utumishi kwa ajili ya utekelezaji huo, ambapo Serikali
imepanga kuajiri walimu wastaafu wenye uwezo wa kufundisha waliokuwa
wanafundisha masomo ya sayansi kwa mkataba ili kupunguza pengo lililopo.
Aidha, Naibu Waziri Jaffo amebainisha kuwa Serikali
inafanya tathimini ya mahitaji ya walimu wa masomo ya sanaa kwa kila
Halmashauri ili kubaini maeneo yenye ziada na yenye upungufu ili kusawazisha.
“Mpango wa Serikali uliopo ni
kuwahamasisha walimu wa ziada wa masomo ya sanaa kwenda kufundisha katika shule
za msingi ndani ya Halmashauri husika, ambapo kabla ya kuanza utekelezaji wa
mabadiliko haya Serikali itatoa waraka maalumu kwenda katika Halmashauri zote
nchini” amefafanua Naibu Waziri huyo.
Akizungumzia kuhusu utaratibu wa mafunzo ya walimu
Mhe. Jaffo amesema kuwa Halmashauri moja haiwezi kuwa na mfumo wa peke yake wa
kuandaa walimu hali ambayo iltakuwa ni vigumu kuthibiti ubora wa mafunzo hayo
kwa walimu.
Hata hivyo amesema kuwa Serikali itaendelea kuongeza
udahili wa walimu wa sayansi katika vyuo vya ualimu kadri watakavyojitokeza ili
kukidhi mahitaji yaliyopo