VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI WAIBUKA NA KUTISHIA MGOMO,WAPANGA KUIBURUZA SERIKALI YA JPM MAHAKAMANI,KISA NI HICHI HAPASOMA HAPO
NA KAROLI VINSENT
VYAMA vya wafanyakazi nchini pamoja na Asasi za kiraia nchini ambayo ipo chini ya mwamvuli wa mtandao wa watetezi wa Haki za Bindamu nchini (THRDC) Wamelitaka bunge la Jamhuri wa muungano wa Tanzania kutopitisha mswaada wa mabadiliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii unaokwenda kuzuia fao la kujitoa,
Hivyo basi wamesema endapo wabunge wakikaidi na kuupitisha mswaada huo na baadae kuwa sheria basi wafanyakazi nchini watagoma ikiwemo kwenda mahakamani kupinga mswaada huo pamoja na kujitoa kwenye mifuko yote ya hifadhi ya jamii kutokana na mswaada huo kumkandamiza mfanyakazi nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam kwa wakati mmoja, na viongozi tofauti wa vyama vya hivyo,ambao ni Gratius Mkoba ambaye ni Rais wa Chama cha wafanyakzi nchini (TUCTA) na pia ni Rais wa chama cha walimu nchini (CWT),Nicomemas Kajungu ambaye ni Katibu mkuu wa Chama cha wafanyakzi wa kwenye migodi nchini na nisharti (NUMET),Bi Majura ambaye ni Katibu mkuu wa chama cha wafanyakzi wa viwandani nchini (TUICO) huku wakiwakilishwa na Onesmo Olenguruma ambaye ametoka (THRDC).
Mkoba amesema wamejitokeza kuupinga mswaada huo baada kujilidhisha kuwa mswaada huo ukupita bungeni na kuja kuwa sheria utakuwa unakuja kumuumiza mfanyakazi kutokana na kutopata stahiki zake anazokatwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
Amesema kitendo cha mfanyakazi kuambiwa makato yake anayokatwa kwenye mifuko hiyo ya kijamii hataruhusiwa kuichukua hadi atapofisha umri wa miaka 60, amedai kuwa jambo hilo ni hatari kwa wafanyakazi na kuzidisha uonevu kwa kwao .
"Tunawaomba wabunge walioangalie hili,ni vigumu sana kuingia kichwani kama leo hii tumefikia hatua ya kutaka mtu anayeacha kazi akiwa na miaka 25 au 30,akae hadi kufikia miaka 60 ndipo achukue poesa zake sawa na yule aliyefanya kazi kwa kipindi cha miaka 60 na kustaafu,hapa inaonekana wameshindwa kuelewa dhana dhima matumuzi ya pesheni,kwani lengo lake ni kumsaidia yule anbapofanya kazi ili maisha yaendelee"amesema Mkoba.
Mkoba amesema Mswaada huu utazidi kuwaumiza hata wafanyakazi wa sekta binafsi ambao wengi wao wamekuwa wanafanya kazi kwa mikataba ya miaka miwili au mitatu akidai kuwa mkataba wake ukiishi kwa kipindi hicho kumfanya asubili hati afike miaka 60 ndio akachukue fedha yake ni kukandamiza na kumnyima fursa.
"Yaani lazima tusimame na tupinge hili kwani watu wengi wanapoaacha kazi wanatumia fedha kujianzisha miradi yao ya maendeleo na kujikimu lakini leo unamvyomtaka achukue akiwa na umri wa miaka 60 ni kumyima fursa,hata wanafunzi wanapomaliza vyuo upenda kujiunga na kazi ya mikataba ili wanamaliza mikataba yao hutumia fedha za mifuko ya jamii kujiendeleza kimasomo"ameeongeza kusema Mkoba.
Kwa upande wake Bi Majura naye amesema hata TUICO Wamesikitishwa na hatua ya serikali kuupeleka mswaada huo kimya kimya bila hata kuwashirikisha wadau wa sekta ya ajira huku akidai kuwa mswaada huo umekuwa na usiri mkubwa jambo analodai linawatia shaka.
Kwa upande wake Kajungu amesema Mswaada huo unatawaumiza hata wafanyakazi wa migodi amabo wengi wao wanafanya kazi kwa mikataba kwani wanaomiliki migodi upewa mikataba ya miaka michache hivyo inawalazimu kuwaajiri wachimbaji migodi wa kwa mkataba hivyo kitendo cha kuwepo kwa sheria hiyo kutawaumiza wafanyakazi wa migodi.
Hata hivyo,Olenguruma amewataka wabunge kuondoa ikadi zao vyama na kuweka mbele maslahi ya wananchi kwa kuungana ma kuupinga mswaada huo kwani haufai kabisa.
"Tunaaamini wabunge wataungana na sisi kuzuia mswaada huo,na kama sauti zetu itapuuzwa,wafanyakazi wanaweza chukua hatua mbali mbali kwama vile kwenda mahakamani,kugoma na kujitoa kwenye mifuko ya kijamii,na waajiri wanaweza sitisha kupeleka michango kwenye mifuko hiyo na kufunga account za mafao hayo hadi hapo usalama wa fedha za wafanyakazi utakapopatikana katika mifuko ya jamii hasa suala la fao la kujitoa"amesema Olenguruma.