TAARIFA MUHIMU KUTOKA TCU,SOMA HAPO KUJUA
Tunapenda kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa
pamoja wa udahili tarehe 31/08/2016 saa sita usiku ili kuchakata maombi ya
waombaji waliofanikiwa kuomba udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Hata hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa
kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu
ya pili kuanzia tarehe 12 hadi 23 Septemba 2016 ili kuruhusu makundi yafuatayo
kuomba udahili.
Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya
kwanza
Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba
katika awamu ya kwanza
Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao
walishindwa kuomba kutokana na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,
Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge”
mwaka 2016 na matokeo yao yameshatoka,
Waombaji waliofaulu mitihani ya RPL,
Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na
uthibitisho toka vyuo vyao vya awali.
Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili
kuruhusu taratibu zingine za kiudahili kuendelea kwa ngazi ya Bodi ya Mikopo na
vyuoni.
Asanteni
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
02 Septemba 2016