ASKOFU AJITANGAZA KUWA NI SHOGA,SOMA HAPO KUJUA
Askofu mmoja wa kanisa la kianglikana nchini
Uingereza amekuwa wa kwanza kutangaza hadharani kuwa anashiriki mapenzi ya
jinsia moja na sasa yuko kwenye uhusiano.
Kasisi Nicholas Chamberlain, amesema kuwa
walioshiriki katika mchakato wa kumteua mwaka uliopita walialewa fika mwelekeo
wake wa jinsia.
''Watu wanajua nashiriki mapenzi ya jinsia moja,
lakini si kitu cha kwanza nachoweza kumwambia yeyote. Jinsia ni sehemu ya yule
niliye, lakini ni kazi yangu ya kitume ambayo ninataka kuiangazia ."
Watu wanajua nashiriki mapenzi ya jinsia moja,
lakini si kitu cha kwanza nachoweza kumwambia yeyote. Jinsia ni sehemu ya yule
niliye mimi, lakini ni kazi yangu ya kitume ambayo ninataka kuiangaziaNicholas
Chamberlain, Asakofu
Nicholas Chamberlain anasema hata hivyo anafuata
kanuni za kanisa zinazosema kuwa haruhusiwi kuoa.
Msemaji wa kanisa la England amesema: "Nicholas
hajamkera yeyote na amekua wazi na mkweli ukiuliza. Suala lake si la siri,
ingawa ni la kibinafsi kama ilivyo kwa wale walio katika mahusiano ya kimapenzi
."
Inadhaniwa kuwa hakuna askofu yeyote anayehudumu
aliyewahi kutangaza hadharani msimamo wake wa kingono.
Kanisa la kianglikana kote duniani limegawanyika
sana miaka ya hivi karibuni kuhusu masuala yanayohusu mwelekeo wa kijinsia na
kutawazwa kwa makasisi walio katika mapenzi ya jinsia moja.