MMILIKI WA STARTV AANZA KUISOMA NAMBA,TRA YAMFANYIA KWELI,NI YULE ALIYEJITOSA KUMSAIDIA JPM KWENYE KAMPENI,SOMA HAPO KUJUA
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imekamata akaunti za
Kampuni ya Sahara Media Group kwa kushindwa kulipa deni la Sh4 bilioni kama
kodi iliyopaswa kulipwa na kampuni hiyo.
Taarifa zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii
zimeeleza kuwa akaunti zote za kampuni hiyo zimefungiwa mpaka pale watakapolipa
deni hilo, lakini kampuni hiyo imetoa ufafanuzi.
Ujumbe huo uliongeza kuwa kampuni hiyo imefikishwa
mahakamani na benki moja hapa nchini kwa madai ya kutaka kulipwa Sh600
milioni, baada ya kuingia makubaliano ya kulipa wafanyakazi wake mishahara
pamoja na mikopo lakini mpaka sasa imeshindwa kurejesha fedha hizo.
Hata hivyo, akizungumzia suala hilo mwenyekiti
mtendaji wa kampuni ya Sahara, Anthony Diallo alikiri mamlaka hiyo
kufungia akaunti ya kampuni yake.
Diallo ambaye ndiye mmiliki wa kampuni hiyo alisema
ni akaunti moja tu iliyofungiwa na kwamba anaamini baada ya kukutana na kufanya
mazungumzo na mamlaka hiyo watafikia muafaka ili biashara ziendelee kama
kawaida.
“Tutalimaliza hakuna kitakachoenda
mrama,” alisisitiza Diallo ambaye aliwahi
kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo nafasi ya Waziri wa Maliasili na
Utalii na Naibu Waziri wa Maji, Maendeleo ya Mifugo katika Awamu ya Nne chini
ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Amesema deni la TRA linatokana na kodi iliyopatikana
baada ya ukaguzi wa vitabu kwa miaka mitatu.
“Ni ukaguzi wa kawaida hufanyika kama
taratibu. Sasa kwa sababu ya kuhamisha matangazo yetu kutoka analojia kwenda
digitali ilibidi tukope benki, ujenzi na kumaliza mradi imechukua miaka
mitatu. Wakati wote tumekuwa tukilipa riba benki na zinazobaki toka mauzo ya
matangazo tunalipa mishahara, umeme na malipo ya kodi za kawaida,”alisema.
“Ni kawaida ila wamefanya hatua za
kutuaibisha tu. Kampuni yetu ya ving’amuzi ni ya Kitanzania na mapato yote
yanaingia nchini wakati kampuni nyingine kubwa zote ni za kigeni kutoka China,
Afrika Kusini, Mauritius na Kenya! Ukweli sisi tunahitaji kusaidia nchi
kiuchumi na kutuharibia ni hasara kwa nchi.”