WATENDAJI WA MAGUFULI WAANZA KUMLUKA MAGUFULI MWENYEWE,AGIZO LAKE KWA MACHINGA LAGEUKWA,SOMA HAPO KUJUA

Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga
katika maeneo ya soko la Kariakoo na barabarani, hususan karibu na barabara za
mabasi ya mwendo kasi.
Akizungumza jana na Kamati ya Bunge, Waziri huyo wa
TAMISEMI alisema kuwa kurejea kwa wafanyabiashara hao katika maeneo hayo
kumeleta usumbufu mkubwa na uchafu wa mazingira katika maeneo ya jiji.
“Namuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
awaondoe na asilegeze kamba,” alisema Waziri
Simbachawene.
Alisema kuwa hali hiyo imetokana na tafsiri isiyo
sahihi ya agizo la Rais John Magufuli alipokuwa ziarani Mkoani Mwanza.
“Wala agizo la Mheshimiwa
Rais halikumaanisha hicho. Mheshimiwa Rais alisema tuwatafutie maeneo mbadala
ambao wapo maeneo kama ya Mwanza na walikuwa wanafanya biashara ya kuuza nguo,
akizungumzia wale particular group walioko pale Mwanza. Kwa Dar es Salaam
tulishamaliza huko,” alisema.
Aidha, alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
kuhakikisha hakuna hata machinga mmoja atakayeonekana akifanya biashara katika
maeneo ya barabara za mabasi yaendayo kasi.
Aigizo hilo la Waziri Simbachawene liliungwa Mkono
na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge ambao walisema kuwa hali ya soko la Kariakoo
imekuwa mbaya kutokana na kuzagaa kwa machinga.