MASIKINI WASIRRA,GWIJI LA SHERIA TUNDU LISSU NA BULAYA WAMZIKA MOJA KWA MOJA KWENYE ULINGO WA SIASA,SOMA HAPO KUJUA
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, imetupilia
mbali maombi mawili yaliyopelekwa kortini kupinga matokeo ya Ubunge wa Jimbo la
Bunda mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana,anaandika Moses Mseti.
Maombi hayo yalipelekwa na
wapiga kura wanne, Magambo Masato na wenzake watatu dhidi ya Ester Bulaya
(Chadema).
Katika kesi hiyo namba moja ya mwaka 2015, maombi
hayo yalipelekwa na wapiga kura hao, kumtetea aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo
hilo, Steven Wassira kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwenye uchaguzi huo
Wassira aliangukia pua.
Uamzi huo umetolewa jana na Jaji Lameck Mlacha,
baada ya kupitia hoja zilizotolewa na Bulaya kupitia wakili wake, Tindu Lissu
kupinga kupokelewa kwa maombi ya wapiga kura hao.
Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, aliweka
mapingamizi matatu ambayo ni kukosewa vifungu vya sheria vya kupeleka maombi
kortini na kifungu cha 10, A na B ambavyo havijatolewa maelezo ya kutosha.
Pingamizi lingine ni kifungu cha 11 kinachotaja
vitendo vya rushwa vilivyofanywa na mfuasi wa Bulaya katika maelezo ya wapeleka
maombi hao lakini hawajavionesha licha ya kumtaja mfuasi huyo.
Katika maelezo ya Lissu kortini hapo, alidai kuwa
katika hoja ya kwanza ya kukosewa vifungu vya sheria kwamba, vimekosewa na
haviipi mahakama nafasi ya kutenda haki na mteja wake kutafuta ushahidi.
Pingamizi la pili Lissu, alidai limekiuka sheria na
hakuna maelezo ya kutosha huku hoja ya tatu ikipigwa chini kwa maana sheria
haimtambui mfuasi bali anayetambuliwa ni mgombea (Bulaya) ama wakala wake ambao
wangetajwa ubunge ungeweza kutenguliwa.
Jaji Mlacha akitolea uwamzi mapingamizi hayo alidai
kuwa, kufuati kupitia hoja za pande zote mbili zilizotolewa Agosti 17 mwaka
huu, anakubaliana na Lissu kwa kufuta hoja ya kwanza na tatu.
Jaji Mlacha amesema kuwa, pingamizi la pili
lililokuwa limewekwa na Bulaya kupitia wakili wake Lissu, anakubaliana naye
katika baadhi ya vipengele ambavyo ni pamoja na wapeleka maombi kushindwa kutoa
maelezo ya kutosha huku akitoa nafasi ya kuendelea kusikilizwa kwa kesi hiyo.
“Paragraph (Aya) ya 11 ilitakiwa kusema vitendo vya
rushwa ambavyo vimefanywa na mfuasi wa Bulaya (Emmanuel Nteleja) na mgombea
(Bulaya) akiwa anafahamu vitendo hivyo licha ya hivyo, aya hiyo ina mapungufu.
“Pamoja na hayo tayari uwamzi katika pingamizi la
kwanza lililokuwa likibishaniwa tayari Jaji Gwae (Mohamed Gwae) alishalitolea
uwamzi na nanuku maelezo yake;
“Mwombaji lazima aoneshe ameleta maombi kwa kifungu
gani na sheria gani ili kuirahisishia Mahakama katika kutoa maamzi,” alinukuu
Jaji Mlacha.
Jaji Mlacha amesema kuwa, kuna baadhi ya vifungu
ambavyo vinaipa mahakama nafasi ya kuendelea kuisikiliza kesi hiyo, huku akidai
kwamba, kesi hiyo itapangiwa siku na Jaji mwingine wa kuisikiliza.
Wakati maamzi hayo yakitolewa kortini hapo, upande
wa mjibu maombi namba moja uliwakilishwa na Wakili Onyango Otieno huku
mlalamikaji ukiongozwa na Wakili Constantine Mtalemwa