WAFANYABIASHARA WA MWENGE WAGOMEA UKUTA YA CHADEMA,SOMA HAPO KUJUA

WAKATI
ikiwa imebakia siku moja ili Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kutekeleza hadha yao ya kufanya maandamano na mikutano ya hadhara nchini kwa
kile wanachosema kupinga Udikteta nchini.
Nao
wafanyabiashara wadogowado wa soko la stendi ya Mwenge Wilaya ya Kinondoni
Jijini Dar es Salaam wamesema hawatashirikia maandamano hayo.
Wamesema
maandamano hayo hayana tija kwa sasa,yanalengo ya kuwagawa watanzania.
Mwenyekiti
wa wafanyabiashara hao ,Omary Hamis amewaambia waandishi wa habari leo Jijini
Hapa wanaungana na Rais John Magufuli katika kile anachokiita ni harakati za
Rais huyo kumkomboa mtanzania myonge,
Amesema
anawambomba vijana wasikubali kurubuniwa
na wanasiasa huku akiwataka kujikita katika kufanya kazi kwa bidii na
kuachana na maandamano hayo.