UROHO WA MADARAKA WAMTESA PROFESA LIPUMBA,AENDELEA KUING'ANG'ANIA CUF ALIYOIKIMBIA,SOMA HAPO KUJUA

Katika
hali isiyokuwa ya kawaida Prof Lipumba ameendelea Kung’ang’ania kiti cha
uenyekiti wa chama chake cha CUF na kusema kikao kilichokaa jana visiwani
Zanzibar na kufanya maamuzi ya kuwasimamisha uanachama, hakikuwa halali na
kilikuwa nje ya katiba ya CUF, sababu mojawapo ikiwa ni kuwekwa kando kwa Naibu
Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya.
“Kikao hicho hakikuwa halali, haiwezekani Baraza Kuu
linakaa halafu Naibu Katibu Mkuu Bara hajui, wala hakujulishwa, na bado kuna
wajumbe wengine hawakuhusishwa” Alisema Prof Lipumba
Lipumba
aliongeza kuwa ni kweli alijiuzulu uenyekiti, lakini baadaye aliamua kuandika
barua kwa Katibu Mkuu ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu na sasa yeye ndiye
Mwenyekiti halali wa chama hicho.
“Nilimuandikia barua ya kurudi kwenye nafasi yangu, akasema
anasubiri ushauri wa kisheria, lakini hadi sasa hakuna kitu, hiyo inamaanisha
kuwa sasa mimi naendelea na nafasi yangu, na niko ngangari kama mwenyekiti” Alisema Prof
Lipumba.
Aidha
aliongeza kuwa alitaka kujieleza katika mkutano mkuu mbele ya wanachama, lakini
mkutano ule ukavurugwa.
Kuhusu
kuwepo kwa tofauti kati yake na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif
Hamad, Prof Lipumba amesema kuwa huenda kuna tofauti kwa kuwa mara nyingi huwa
hamuelewi jinsi anavyokiendesha chama bila kifuata misingi ya kidemokrasia.
“Katibu Mkuu anamdharau na hampi heshima yake Naibu Katibu Mkuu
Bara, mara nyingi huamua mambo yake bila kushirikisha viongozi wengine, halafu
sasa anataka kufukuza wanachama, huwezi kuwa na chama halafu ufukuze wanachama,
wanachama wanatafutwa duniani kote, halafu wewe unawafukuza, hizo ni dalili za
uongozi wa kiimla, kuongoza chama unapaswa kujali demokrasia na siyo kuwa
dikteta ndani ya chama” Amesema
Kuhusu
Julius Mtatiro kuwa mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uongozi, Lipumba amesema kuwa
hatambui maamuzi hayo, na wala hamtambui Mtatiro kama kiongozi wa chama hicho
bali mjumbe wa Mkutano Mkuu, nafasi ambayo yeye ndiye aliyempa.
“Mtatiro hawezi kuwa mwenyekiti, mimi ndiye mwenyekiti wa chama,
Mtatiro alishindwa hata kuongoza mkutano mkuu, ukavurugika, hawezi, simtambui”