WASAIDIENI WANAFUNZI WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU,SOMA HAPO KUJUA
JAMII imehaswa kuwasaidi wanafunzi wanaoishi
mazingira magumu ili waweze kujikwamua kielimu .Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Wito huo umetolewa
Jana Jijini Dar es Salaam na Bleesing Hamed Mlanga ambaye ni Mwanzilishi
wa Mpango wa kuwasadia wanafunzi waoishi kwenye mazingira magumu wakati mkutano
wa kuchangia pesa kwa ajili ya wanafunzi hao.
Amesema Jamii inapaswa kujitolea kwa ajili ya
kuwasaidi wanafunzi wenye mazingira magumu ili waweze kujikwamua kelimu ili
jamii iweze kusonga mbele.
Amesema sababu inayomfanya yeye kujitolea kuwasaidi
wanafunzi hao imetokana na yeye kuwa muhanga wa matatizo ya mazingira magumu
jambo analodai linatakiwa kuungwa mkono na kila mtanzania.
Aidha,Mlanga amesema kwa sasa mpango huo
aliouanzisha umewasaidia kupata bei zaidi ya 100 ya viatu kwa ajili ya
wanafunzi ambao wanakwenda shule bila viatu ili waweze kuvaa viatu hivyo.
Kwa upande wake Zuber Samataba ambaye ni Katibu
Tawala Mkoa wa Pwani. amesema jamii inatakiwa kujitolea katika kuisaidia katika
elimu ili wanafunzi wanaweze kupata elimu bora.
Amesema licha ya serikali ya awamu ya tano kufanya
juhudi katika kutoa elimu bule kwa wanafunzi lakini amedai kuwa bado jamii
itakiwa kuonyesha mshikamano katika kusaidia wanafunzi wenye mazingira magumu.