Zinazobamba

MZEE WA UPAKO AFUNGUKA NA KUELEZA HAYA KUHUSU MAGUFULI,AISIFIA CHADEMA,SOMA HAPO KUJUA



 
MCHUNGAJI wa Kanisa La Maombezi (CRG), Antony Lusekelo (maarufu mzee wa upako) amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ni chama cha upinzani kinachokuwa kwa kasi huku akisema  Chadema ya sasa sio ya 1992 .Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Hata Hivyo,Lusekelo ameonyesha masikitiko yake kwa jeshi la Polisi nchini kujikanyaga katika kuzuia mikutano ya kisiasa hususani vyama vya Upinzani kwa kusema  jeshi hilo linajijengea picha mbaya kwa jamii kwa kuonekana linakipendelea chama cha Mapinduzi CCM ambapo amedai hali hiyo inaweza kuzaa mtafaruku ndani ya jamii.

Kiongozi Huyo wa Kiroho ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ambao walimtembelea kanisani kwake Ubungo Kibangu jijini hapa, ili kuzungumzia hali ya kisiasa nchini.

Amesema  kwa sasa upinzani nchini umekuwa kwa kasi huku akiwataka viongozi waliopo madarakani kufanya kazi kwa ushirikiano na vyama vya upinzani ili nchi iweze kupiga hatua.


“Kwa sasa uchaguzi umekwisha ni vema viongozi walioko madarakani wakafanya kazi na vyama vya upinzani,na nashangaa watu wanaokibeza Chama cha Chadema,Chadema ya sasa sio chadema ya 1992 ilipoanzishwa,hii chadema ya sasa wananchi wanaimani nayo kiasi kikubwa ndio maana wameipa wabunge zaidi 40”amesema Lusekelo.

Amesema baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 nchi yetu bado haijatulia vyema kwa kile anachokiita bado kuna majeraha ya uchaguzi huku akiwataka  viongozi mbali mbali kutumia mwaka wa 2016 na 2017 kuziba majeraha hayo.

“Uchaguzi ule ulikuwa uchaguzi mkubwa tulishuhudia vyama kuwa na makundi,tuliona hata mafuriko ya watu kwenye kampeni,msifikili watu wale wamekufa au wamepotea wale watu wapo hamjui wanafikiria nini,kwahiyo ni vema sana tukaungana kwa pamoja kuliombea taifa ili tuwe kitu kimoja “Alisema
Hata Hivyo,Lusekelo amesema hatua ya Jeshi la Polisi kukataza vikao vya kisiasa vya Vyama vya Upinzani  na wakati huo huo linaibuka na kuruhusu mikutano ya ndani ya CCM ni mapungufu yanayotokana na katiba ya sasa ambayo inampa Mamlaka Rais kumteua mkuu wa jeshi la Polisi (IGP) .
“Ndio maana hata mimi siwezi kabisa kuingia kwenye siasa za nchi hii,kwani Polisi wanafanya kazi kwa uoga huyu IGP anateuliwa na Rais,na Rais huyo huyo ni Mwenyekiti wa CCM sasa unategemea IGP anauwezo wa kumzuia alimyemtua" Alihoji

KUHUSU MGOGORO UNAOENDELEA NDANI YA BUNGE.
Lusekelo amesema hatua ya wabunge wa vyama vya Upinzani wanaounda vyama vya Ukawa kususiasa Vikao vya Bunge inatoka na zote mbili baina ya Wabunge wa Upinzani na wabunge wa CCM kuwa wabinasfi
 Amesema hata, Naibu Spika wa Bunge pia ameonekana kuwa mchanga  katika kisiasa, hivyo akawaomba wazee kuingilia kati ili  kuweza kuumaliza mgogoro huu.
“Huyu Naibu spika ni mchanga sana kwenye siasa,harafu hajachaguliwa kwa kura kutoka kwa wananchi,ni wakati wa wazee wakongwe kama wakina Pinda,Mzee Salim pamoja na James Mbatia kukutana na kumaliza mambo ili Taifa letu lisonge mbele”amesema Lusekelo.
 Vilevile Lusekelo amesikitishwa na hatua ya mikutano ya Bunge kutorushwa moja kwa moja huku akisema kitendo hicho kimewanyima fursa watanzania kupata haki yao ya msingi huku akidai kitendo hicho kitazidisha uvivu wa wabunge kulala na kushindwa kutoa hoja.
   HATUA MBALI MBALI ANAZOCHUKUA RAIS JOHN MAGUFULI.
Lusekelo amesema hatua anazochukua Rais Magufuli za kukusanya kodi kwa wingi,kupambana na Ufisadi vinatakiwa kuungwa mkono huku pia akiwasihi watanzania kuwa na uvumilivu na ugumu wa maisha uliopo sasa kwa kutoa utabili wake kuwa mambo yatakuwa mazuri baada ya mwaka mmoja na kila mtanzania atajivunia na utawala huu.

“Leo kila mtu analalamika maisha magumu,hata nyie waandishi jiulizeni tangu aingie madarakani ameshawai kutoka hata nje ya nchi huyu magufuli,yupo ndani ya nchi anapanga mikakati ya kuweza kuwaletea maendeleo wananchi,nataka niwaaambieni baada ya mwaka mmoja kila mtanzania atafurahia hali ya nchini”amesema Lusekelo.
  KUHUSU LAWAMA KWA VIONGOZI WAASTAAFU.
Pia amezungumzia kuhusu shutuma mbali mbali zinatolewa na watu mbali mbali kwa viongozi waastaafu kuwa wanamiliki mali nyingi huku akiwatetea kwa kusema kwa Afrika yetu ilivyo viongozi waastaafu hapa nchini   wana  hali ya chini tofauti na nchi zengine.
“Mimi nimetembea zaidi ya 14 hapa afrika,jamani hawa viongozi wetu waastaafu wanamaisha ya kawaida sasa,hebu mwangalie mzee Sumaye,Warioba,Malecela,hawa wanamaisha ya kawaida sana ni vema wakaachwa tu,ingekuwa viongozi wa nchi zengine Afrika wangekuwa na mali nyingi sana”amesema Lusekelo.
  UJIO WA TB JOSHUA NCHINI.
Lusekelo ametoa taadhari kwa nchi kutompokea tena mhubiri maarufu kutoka nchini ya Nigeria TB Joshua kwa kile alichosema atasababisha maafa makubwa kutokea nchini kwa madai kuongozi huyo hana sifa ya kuwa mhuburi.
“Huyu Tb Joshua afai hata kidogo ni mtu mwongo ambaye anafaa kuzuiliwa,ni mtu muongo hivyo endapo Rais Magufuli akienda kumpokea tena huyu Tb Joshua basi yatatokea maafa makubwa sana nchini”amesema Lusekelo.