ANTONY LUSEKELO ATAKA WANASIASA KUTIBU MAJERAHA YA UCHAGUZI WA 2015, APINGA TB JOSHUA KUPOKEWA NA RAIS MAGUFULI
SELEMANI MAGALI-DARESALAAM
MCHUNGAJI wa Kanisa La Maombezi
(CRG), Antony Lusekelo (maarufu mzee wa upako) amewataka viongozi wa Kisiasa
hapa nchini kuacha tabia ya kupigana vijembe katika mikutano yao ya chama badala
yake wajikite katika kutibu majeraha ya uchaguzi wa mwaka jana kwa kuhubiri
ushirikiano na umoja wa kujenga Taifa.
Amesema si wakati wa kubeza
baadhi ya watu waliohama chama kimoja kwenda kingine, kwani kufanya hivyo
kunajenga chuki miongoni mwa jamii na hivvyo kuhatarisha Amani ya nchi
iliyojengwa kwa miaka mingi
Hayo ameyasema leo wakati
akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea ofisini kwake kwa lengo la
kuzungumza mwenendo wa Kisiasa hapa nchini na ushauri kama kiongozi wa kiroho
hapa nchini.
Lusekelo amesema kwa muda mrefu
amekuwa akifuatilia siasa za hapa nchini na amekuwa kimya kwa muda lakini
ameamua kuyasema hayo ili kuendeleza Amani ya Tanzania
“Nimeona kumeanza kujitokeza
vijembe miongoni mwa wanasiasa, kuna wanaowakejeli wwenzao kwa kuhama chama
kimoja kwenda kingine lakini pia kuna wanaofikia hatua ya kuwasema vibaya
wenzao, nadhani huo si utaratibu mzuri na si utamaduni wa Tanzania”Alisema.
Amesema kwa sasa upinzani nchini umekuwa kwa kasi, na
unawafuasi wengi kitendo cha vijembe vitasababisha machafuko ambayo hayana
ulazima wowote.
“Baada ya uchaguzi mkuu wa 2015
nchi yetu bado haijatulia vyema, bado watu wanamajeraha makubwa ya uchaguzi
mkuu, ni wakati wa kuponya majeraha kwanza tena kwa miaka miwili 2016 na ule wa
mwaka 2017, tuhubiri umoja” Alisema
Aidha
akizungumzia kuhusu vitendo vya wabunge wa upinzani kususia bunge,Mchungaji Lusekelo
amesema kitendo kile kinatia aibu taifa, na ameshauri wazee wajitokeze ili
kusawazisha mambo na ili Taswira ya Taifa isiharibiwe.
“Amesema hakuna wa kulaumiwa kilichotokea
bungeni Dodoma, wote wanamakosa kuanzia wabunge wateule na hata Naibu Spika wa
Bunge Bi Tulia Ackson, na hiyo inatokana na uchanga,
kinachotakiwa wazee waingilie kati ili suluhisho lipatikane” Alisemapia
AMVAA
TB JOSHUA WA NIGERIA
Katika
hatua nyingine Mchungaji Lusekelo ameitahadharisha Serikali ya awamu ya tano
kuacha kumpokea Nabii TB Joshua wa Nigeria kwani kufanya hivyo kutasababisha
laana kubwa kwa Taifa la Tanzania ikiwemo kunyesha mvua sizizo fahamika.
Amesema
TB Joshua hana unabii wowote, Zaidi anadanganya umma wa wananchi wanahudhuria
katika kanisa lake,lakini hana lolote ambalo linawashinda wachungaji wa
Kitanzania wanaotangaza injili kwa lugha ya Kiswahili.
“Nimesikia
ati TB Joshua anakuja Nchini na anatarajiwa kupokelewa na Rais Magufuli…nataka
nimwambie Rais Magufuli kumpokea TB Joshua ni kuleta laana katika Taifa. Hana la
ziada ambacho wachungaji wa ndani hawana.”Alisema
Lusekelo
ametoa taadhari kwa nchi kutompokea tena mhubiri maarufu kutoka nchini ya
Nigeria TB Joshua kwa kile alichosema atasababisha maafa makubwa kutokea nchini
kwa madai kuongozi huyo hana sifa ya kuwa mhuburi.
“Huyu
Tb Joshua afai hata kidogo ni mtu mwongo ambaye anafaa kuzuiliwa,ni mtu muongo
hivyo endapo Rais Magufuli akienda kumpokea tena huyu Tb Joshua basi yatatokea
maafa makubwa sana nchini”amesema Lusekelo.