CHADEMA YAWATOLEA UVIVU WANACHAMA WAKE WALIORUDI CCM,YASEMA HAYA ,SOMA HAPO KUJUA
Wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM jana mjini Dodoma,
Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kiliwapoteza wanachama wake watatu
baada ya kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wanachama hao waliokihama chama hicho ni Fred
Mpendazoe ambaye alikuwa mwanachama wa CCM pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kishapu
mwaka 2005 hadi 2010 kupitia CCM, Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Singida na mbunge wa zamani wa Iramba Mashariki na mwigizaji wa filamu
nchini Tanzania Jackline Wolper.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA
alipohojiwa jana wakati kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinaendelea alisema
kuwa, hawana muda wa kukaa na kuanza kumjadili mtu mmoja mmoja anayesemekana
kuhama chama hicho.
"Kamati Kuu ni kikao kizito sana,
hatuwezi kuacha kujadili masuala ya msingi na kuanza kuwajadili hao
wanaosemekana kuwa wamehama chama," alisema
mjumbe huyo.
Kamati Kuu ya CHADEMA imekutana jana na leo katika
vikao vya dharura ikiwa na lengo kubwa la kujadili mwenendo wa hali ya kisiasa
nchini.