WANAFUNZI "VILAZA" WA MAGUFULI UDOM,MAPYAA YAIBUKA SERIKALI YAJA NA HILI,SASA WATAKIWA KUREJESHA FEDHA ZA SERIKALI,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
WAKATI Rais John Magufuli na Rais mastaafu wa awamu
ya nne Jakaya Kikwete wakiwa wanatofautiana
kuhusu wanafunzi 7805
waliokuwa wanasoma stashahada maalumu ya Ualimu wa Sayansi na Hisabatii katika
chuo kikuu cha Dodoma,
Huku Rais Magufuli akisema wanafunzi wa hao ni
"vilaza" na hawana sifa ya kusoma hapo huku pia naye mtangulizi wake Rais mstaafu
Kikwete akisema wanafunzi hao wana sifa za kusoma chuoni hapo.
Nayo,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ni kama
imetengua ubishi huo baada ya kusemwa kati ya wanafunzi 7805 waliokuwa wanasoma
huo hicho ni wanafunzi 382 ndio wanatajea chuoni hapo baada ya kubainika kuwa wamekizi vigezo.
Huku Wanafunzi 5922 watahamishiwa kwenda kwenye
vyuo vya ualimu vya serikali na kuendelea na kusoma ngazi ya cheti.
Pia wizara hiyo imesema wanafunzi 290 ambao wamegundulika hawana sifa za kusoma ngazi hiyo, wametakiwa kwenda
kwenye vyuo vyenye hadhi yao na kuanza kusoma upyaa baada ya kugundulika kupata
daraja la nne huku wakikosa sifa husika.
Hata Hivyo,pia Wizara imesema wanafunzi hao ambao
walikuwa hawana sifa ambao walikuwa wananufaika fedha za kujikimu za kila siku walizokuwa
wanalipwa pindi walipokuwa wanasoma Dodoma wanatakiwa kuzirejesha haraka .
Profesa Joyce Ndalichako ambaye Waziri wa
Elimu,Sayansi na Teknolojia amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa
mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema mara baada ya 28 Mei serikali kuwarejesha nyumbani wanafunzi
hao,ndipo serikali ilipoamua kuchunguza wanafunzo hao na kupata ukweli juu ya
vyeti vyao.
Amesema katika uchambuzi huo iligundulika wanafunzi
wa stashahada ya ualimu wa sekondari waliopata daraja la kwanza katika kidato
cha nne ni 37 daraja la pili 354 daraja
la tatu 6183 huku pia lilikuwepa daraja la 4 walikuwepo 21 jumla yake ni 6595,
Amesema licha ya mwongozo wa kusoma kozi hiyo
maalumu ilikuwa ni kwa ajili ya waalimu wa sekondari tu,
lakini ameshangazwa pia kuwepo kozi ya
Stashahada ya Ualimu ngazi ya Msingi
ambayo ikiliwa na wanafunzi 1210 ambapo ni kinyume na ilivyokuwa
inatakiwa .
“Wanafunzi 6595 walidahiliwa kusoma program ya
stashahada Maalum ya Ualimu wa Elimu ya sekondari kwa masomoya hisabati na
sayansi kati yao 6305 walikuwa na sifa
stahiki ambazo ni ufahulu wa daraja la 1 hadi la tatu na ufahulu ulikuwa kwa kiwango cha gredi C hadi A katika
masomo mawili ya sayansi ndivo sheria inavyotaka”ameelezaProfesa Ndalichako.
Amesema hata hivyo pia kulikuwepo na makosa ya
kudahili wanafunzi wa walipata daraja la nne ambao walikuwa 52 ambapo ni
kinyume na sheria inavyotaka kwani walikuwa hawajakizi vigezo.
Profesa huyo amesema hata wanafunzi 269 walikuwa na
ufahulu wa daraja la 1 hadi la tatu lakini wamegundulika walikuwa hawajafahulu kiwango
cha A hadi C kwa masomo mawili ya Sayansi .
“Yaani hii pogramu ilikuwa ni ya walimu wa Sayansi
na Hisabati lakini tumekuta hadi wanafunzi wanaosomea stashahada za ualimu wa
masomo ya Biashara wakati ni tofauti na inavyotaka mwongozo”amesema Profesa
Ndalichako ,
MAAMUZI YA
SERIKALI BAADA YA UCHUNGUZI HUO.
Waziri Ndalichako amesema serikali baada ya kupitia
kwa makini majina ya wanafunzi hao wameamulu kuwa wanafunzi 382 ambao ni kundi
la stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari ambao wamepata daraja la
kwanza na pili ambao pia wamehahulu katika masomo mawili ya sayansi na hisabati
ndio wataruhusiwa kujerejea kusoma chuoni hapo.
Huku pia wanafunzi 4,586 wa mwaka 1 wa program Maalum
ya stashahada ya ualimu wa Elimu ya sekondari waliokidhi vigezo vya ufahulu
watahamishiwa katika vyuo vya ualimu vya Morogoro,Butimba,Mpwapwa,Songea na
Tukuyu ili wakamalizie masomo yao.
Hata hivyo,wanafunzi 1,337 wa mwaka wa pili
watahamishiwa kwenye vyuo vya Ualimu vya korogwe na Kasulu kumalizia masomo
yao,
Huku wanafunzi 290 ambao hawakuwa na sifa ya kusoma
chuoni hapo wametakiwa kuanza kuomba upya kwenye vyuo vyenye hadhi yao.
Vilevile,Waziri
Ndalichako ameagiza wanafunzi wote ambao walikuwa wananufaika na pesa za
kujikimu ambao wamegundulika hawa sifa ya kusoma kozi hiyo wametakiwa
kuzirejesha fedha hizo kama sheria inavyotaka.
Pia kwa wale wanafunzi ambao watahamishiwa kwenye
vyuo vya elimu serikali itawalipia fedha ya ada ya laki sita huku fedha hizo
kulipwa moja kwa moja kwenye chuo hisika na sio kupewa mwanafunzi.