RAIS MAGUFULI AIBUA UFISADI WA KUTISHA NDANI YA JESHI LA POLISI,SOMA HAPO KUJUA
Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha
na vitendo vya rushwa ambavyo vilinafanya jeshi hilo kukosa heshima katika
jamii huku akisema kuwa ana taarifa za jeshi hilo kuingia katika makubaliano ya
kifisadi ya mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kununua sare za jeshi hilo.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa
akiwaapisha makamishna wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo na kuongeza kuwa
ni jambo la kusikitisha kwamba mabilioni hayo yalitolewa kwa siku moja lakini
hadi leo hakuna hata sare moja ya iliyonuuliwa.
Ameshangazwa na jeshi hilo kutoa kiasi cha fedha
kinachokadiriwa kuwa kati ya shilingi bilioni 40 hadi 60 kwa ajili ya sare za
polisi ambazo hadi leo hakuna hata moja iliyonunuliwa na wakati huohuo jeshi
hilo likikosa shilingi bilioni 4 tu za kukomboa magari yao zaidi ya 70
yanayoshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huko bandarini.
Aidha, Rais Magufuli ameagiza uchunguzi ufanyike na
wahusika wafikishwe mbele ya haki ila angalau hata nusu ya fedha hizo ziweze
kurudishwa zikalipie magari ya polisi yaweze kutoka bandarini maramoja.
Amelitaka pia Jeshi la Polisi kuachana na utaratibu
wa kuwa na watumishi ambao ni raia wa kawaida na badala yake polisi wenyewe
ndio washike nafasi hizo kulingana na taaluma husika na kushangazwa na taarifa
kuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi aliyetumbuliwa hivi karibuni kwa tuhuma za
ubadhirifu alikuwa raia wa kawaida na sio polisi.