MAKONDA ATISHIWA MAISHA NA MASHOGA,SASA AVIANGUKIA VYOMBO VYA ULINZI,SOMA HAPO KUJUA
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema
tangu alipotangaza kuanza kukamatwa kwa mashoga, amebaini kuna mkakati
unawaohusisha watu hao zaidi ya 150 kutaka kumwangamiza.
Kauli hiyo aliitoa jana Dar es Salaam baada ya
kumaliza mahojiano katika kituo cha redio Clouds FM, ambako alikuwa akifafanua
hoja na changamoto mbalimbali za mkoa wake.
Alisema kuwa baada ya kubainika kwa mipango hiyo,
mashoga wanane wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi.
“Lazima watu wajue jitihada na harakati
za kusimamia katiba na usawa hapa nchini. Hakuna anayezipenda, vita inakuwa
kubwa… Nimebaini kuwa mashoga zaidi ya 150 waliketi katika baa moja Kinondoni
wakipanga njama za kunimaliza kwa namna moja ama nyingine, lakini
kutokana na taarifa za kiintelijensia, watu kadhaa, wengi wao wakiwa ni
mashoga wameshakamatwa,” alisema Makonda.
Katika hatua nyingine, Makonda aliwatolea uvivu watu
wanaosambaza ujumbe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii,
ikiwamo kutengeneza akaunti feki.
“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina
akaunti ambayo inaanza na cheo changu, hivyo akaunti zote zangu zimeandikwa kwa
jina langu Paul Makonda si vinginevyo, hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo,”alisema
Makonda.
Aliweka wazi kuwa kuna agizo batili lililowekwa
katika mitandao ya kijamii, akidaiwa kusema kuwa watu wasiokuwa na kazi
watakwenda jela, lakini ukweli ni kwamba ameagiza wenyeviti wa Serikali za mtaa
kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya
usalama wa maeneo wanayoishi.
Aidha Makonda alisisitiza kuwa kutokana na matatizo
yaliyopo, kamwe Hatoacha kupambana na mafisadi katika halmashauri zote tatu za
mkoa wake, pamoja na wauza unga, wafanyabiashara wa shisha na mashoga.