MKUU WA MKOA WA DODOMA AJIKOMBA KWA RAIS MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
Jordan Rugimbana, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma |
WAKATI ‘mzuka’ wa Baraza la Vijana wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) ukishuka baada ya kusitisha kusudio lao la
‘kuisaidia’ polisi kutekeleza agizo la Rais John Magufuli pia Jeshi la Polisi
nchini, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma naye amejitosa, anaandika Dany Tibason.
Jordan Rugimbana, Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma amekuja na tamko lake leo kwamba, mtu au kikundi ambacho kinadhani
kufanya fujo katika mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ‘atakula naye
sahani moja’ kwani Dodoma si salama kwa watu wenye nia ovu.
Rugimbana
anatoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya viongozi wa Bavicha
kutangaza vijana wake kutulia amri ambayo iliyoka kwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti
wa Chadema Taifa.
Kumekuwepo
na vuta nikuvute kwa takribani wiki tatu kati ya Jeshi la Polisi na Bavicha pia
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuhusu kuzuia mkutano huo kwa mujibu wa maelezo
ya polisi kwamba, hali nchini hairidhishi.
Wakati
muafaka ukiwa tayari umepatikana kabla ya mkutano mkuu maalumu wa CCM kuelekea
kumkabidhi madaraka ya uenyekiti wa CCM Dk. Magufuli kutoka kwa mwenyekiti wa
sasa Dk. Jakaya Kikwete, Rugimbana amejitokeza na ‘kunogesha’ kuwa, Dodoma si
mahala pa uovu.
Ametoa
kauli hiyo leo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya
shughuli mbalimbali za kitaifa ambazo zinatarajiwa kufanyika mapema mjini humo.
Amesema,
kutokana na kuwepo kwa matamshi mbalimbali ya baadhi ya vikundi kudai kuwa,
vina malengo ya kuzuia mkutano wa CCM, ametaadhalisha kuwa, kwa sasa
Mkoa wa Dodoma “siyo salama kabisa kwa mtu au kikundi cha watu ambao wanadhani
wanaweza kuonesha umaarufu wao au kufanya fujo katika mkutano huo.”
Rugimbana
ambaye kwa Mkoa wa Dodoma ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama amesema,
kamwe katika kipindi hiki na kipindi chochote kile Dodoma haitaweza kuruhusu
watu kuchezea amani iliyopo.
Licha
ya kutokutaja majina na vikundi hivyo wala mtu yoyote lakini inaonesha wazi
kuwa, kauli ya Rugimbana inailenga Bavicha ambao awali walitangaza msimamo wao
wa kutaka kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa lengo la kuzuia mikutano yote ya
kisiasa ili kutimiza lengo la Rais Magufuli.
“Nawatangazia
Watanzania wote hasa wale ambao wana nia ya kufanya fujo au kikundi cha watu
ambao wana nia ya kufanya fujo katika mkutano mkuu wa CCM, wasijaribu kabisa
hata kama wapo ambao wameonekana kukiri na kufuta nia yao ya kutaka kufanya
zuio katika mkutano wa CCM lakini hatuwezi kufumbia macho.
“Kwa
Mkoa wa Dodoma ulinzi upo wa kutosha na anayedhani kuwa anaweza kufanya fujo,
kuonesha umaarufu wakae wakijua kabisa kuwa Dodoma ya leo siyo salama kwao,”
amesema Rugimbana.
Wakati
huo amesema, katika Mkoa wa Dodoma kwa sasa kuna matukio makubwa ambayo
yanaufanya mkoa kuwa na viashiria vya kuwa Makao Makuu.
Ametaja
shughuli hizo kuwa ni kesho saa 10 jioni Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu
anatarajiwa kuzindua ujenzi wa uwanja wa ndege kwa awamu ya kwanza kwa niaba ya
Rais Magufuli.
Amesema,
upanuzi huo wa uwanja wa ndege unaozinduliwa na Waziri Mkuu ni kwa ajili ya
kuwezesha usafiri wa anga kuwa mwepesi na kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa na
wepesi wa kufikiwa.
“Tumekuwa
na mtandao wa barabara,lakini hatukuwa na uwanja wa ndege wa kupokea ndege
kubwa lakini kwa sasa tutakuwa na uwezo wa kutumia ndege na kwa njia hiyo fursa
kubwa ya wafanyabiashara na watu wengine kutumia uwanja wa ndege” amesema
Rugimbana.
Kwa
hatua nyingine amesema, maandalizi ya ujenzi wa Viwanja vya Mashujaa pamoja na
kujenga mnara kwa maana ya kusherekea sikukuu ya mashujaa, yanaendelea vizuri
na kuwa, kwa mara ya kwanza yatafanyika mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa
Rais Magufuli.
Amesema,
katika maandalizi hayo ya mashujaa, mashujaa wameisha fika katika viwanja hivyo
kwa ajili ya kufanya mazoezi.
Kutokana
na ugeni mkubwa ambao hupo mkoani hapa Rugimbana amewataka watoa huduma
mbalimbali kuhakikisha wanatoa huduma bora ambazo zitakuwa zikiwaridhisha
watumiaji.
HALI YA DODOMA
Matamko
mbalimbali ambayo yanatolewa na Bavicha yameonesha wazi kuwatia kiwewe viongozi
wa CCM na kulazimika kuwa na ulinzi mkali.
Katika
hali isiyokuwa kawaida, ulinzi umeimarishwa zaidi tofauti na mikutano mikuu
yote ya CCM kutokana na jengo la CCM Makao Makuu kuzungukwa na walinzi ambao ni
vijana wa CCM.
Kwa
kawaida jengo la CCM Makao Makuu lima milango mitatu ambao mlango mmoja mkubwa
ni kwa ajili ya kupitisha magari, mlango mdogo upitiwa na watu kwa njia ya
kawaida hususani waandishi wa habari na mlango mwingine hutumiwa na watu wote.
Hata
hivyo, kwa siku ya leo imekuwa tofauti kwani kila kona kuna ulinzi huku UVCCM
wakiwa wanafanya ulinzi kwa kuzuia njia ambazo zinatakiwa kupitiwa.