TECNO WAZINDUA SIMU KALI YA CAMON C9
MENEJA MAUZO KUTOKA KAMPUNI YA TECNO MOBILE FRED KADELANE AKIONYESHA SIMU HIYO MARA TU BAADA YA KUZINDUA. WATEJA MIA MOJA WA KWANZA WALIFANIKIWA KUPATA SIMU ZAO. |
Tecno Mobile imezindua simu mpya aina ya CAMON C9 yenye uwezo wa hali ya juu katika kupiga picha, uwezo wa 4G LTE na teknolojia mbali mbali za kisasa
Tecno Camon C9 iliyoanza kuuzwa
toka tarehe 25 Juni 2016. Ina uwezo wa hali ya juu katika suala zima la kupiga
self na kwamba ni simu ya kijanja inayoendana na kasi ya mabadiliko ya
Teknlojia ya simu.
Akizindua simu hiyo meneja mauzo
toka Tekno Fredy Kadelane amesema simu hiyo imekuja kukidhi haja ya wateja
wanaotaka vitu vyenye viwango vya juu, akisistiza simu hiyo kuwa ni Zaidi ya
simu.
“Kama mpenzi wa picha Camon C9
imekupa Camera unayoihitaji kwani inaweza kutambua sura na kupiga selfie kali
hata ukiwa gizani. Pia Camera yake ina urembo wa kweli (make-up) ambayo
itafanya picha zako kuwa na mvuto wa asili.” Alisema Kadelane
Ameongeza kusema Tecno Camon C9 ina uwezo wa kujaza watu wengi kwenye selfie moja jambo ambalo ni tofauti na simu yoyote ile duniani. Camera ya C9 inachukua angle kubwa zaidi hivyo kukuwezesha kupata selfie nzuri ya watu wengi zaidi.
Ametaja sifa nyingine ya Simu ya Camon C9 kuwa ina Iris recognition Inayosaidia
mmiliki wa simu kuweza kufunga simu yake na kufungua kwa njia ya kuitazama
badala ya kuweka neno la siri (Password) kama ilivyozoeleka katika simu zingine.
“Sasa hakutokuwa na sababu ya
kuweka password, Tecno inatumia teknolojia mpya ya IRIS recognition ambayo
inatumia macho kufungua simu. “ alisema
WATEJA 100 WA KWANZA WAPEWA SIMU
ZAO
Aidha wateja 100 wa kwanza ambao
walifanya zoezi la ku order mapema simu hizo wamefanikiwa kupewa simu zao
katika showroom ya Tecno iliyopo duka la City Mall jijini Daresalaam.
“Uzinduzi huu unaenda sambamba
na kutoa simu kwa wateja wetu miamoja wa kwanza waliyofanya manunuzi ya awali
(pre-order) katika show room zetu zilizopo City Mall, Clock tower na Mobile
plaza ghorofa ya pili.”Alisema
Aidha akifafanua jinsi wateja wa
awali walivyoshiriki kufanya manunuzi ya awali, Amesema wateja hao walifanya
malipo ya awali ya Tsh. 30,000 na kupewa kadi ya “huduma kwa wateja kutoka”
Tecno na kifurushi cha zawadi (gift hamper) za bidhaa kutoka Tecno.
Kadi ya huduma kwa wateja
itatumika katika kutengenezewa simu katika duka zetu za Tecno baada ya kujipatia
simu yenyewe.
WATEJA WAIPA KONGOLE TECNO MOBILE
Kwa upande wao wateja waliofika
katika duka la city mall kuchukua simu zao hawakusita kuonyesha furaha yao
baada ya kupokea simu hizo wakisema simu hizo zinaendana na wakati wa sasa na
kwamba gharama yake ni nafuu ukilinganisha na ubora wa simu yenyewe.
Akizungumza na Fullhabari.com,
mmoja wa wateja hao Bw.Harrison Ndungulile amekili kwa kusema simu hiyo ya
common c9 imekuja kukidhi haja za watu wanaopenda zimu za smartfone
Hakuna maoni
Chapisha Maoni