CUF YAZINDUA TAWI LA WANAFUNZI WANACHAMA WA CUF LA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (JIVICUF UDSM)
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa , Juvicuf, ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobal (kushoto), akizungumza na wanafunzi wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (JIVICUF UDSM), Dar es Salaam jana wakati akizindua tawi la wanafunzi hao katika chuoni hapo.
Mbunge wa Kilwa Kusini Seleman Bungara maarufu Bwege (CUF), akizungumza na wanafunzi hao katika uzinduzi huo.
Mbunge wa Liwale Zubeir Kuchauka (CUF), akichangia jambo kwenye mkutano huo wa uzinduzi.
Mwongozaji wa uzinduzi wa tawi hilo, akiwa kazini.
Mbunge wa Viti Maalumu (CUF) kutoka Pangani akichangia jambo.
Taswira meza kuu katika uzinduzi huo.
Wanafunzi hao wakiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa , Juvicuf, ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobal (kushoto), akikabidhi kadi kwa wanafunzi hao.
Kadi zikitolewa.
Kadi zikiendelea kutolewa.
Hapa ni wanafunzi hao wakiwa na furaha baada ya kukabidhiwa kadi
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa , Juvicuf, ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobal (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi hao baada ya kuzindua tawi hilo.
Picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa kadi za kujiunga na umoja huo.
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimezindua Tawi la Wanafunzi wanachama wa CUF la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Jivicuf UDSM), ikiwa ni moja ya mikakati ya kujitanua kisiasa kwa chama hicho.
Uzinduzi huo umefanywa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa , Juvicuf, ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobal, Dar es Salaam jana ambapo aliwataka vijana kutumia ujana kupigania haki na demokrasia nchini
Alisema pamoja na kupigiani haki hasa za wanyonge vijana pia wanapaswa kushika nafasi mbalimbali za uongozi ili kusimamia rasilimali za nchini na wananchi.
"Nimezindua tawi hili la Juvicuf UDSM, nawataka mfanye siasa za nidhamu lakini msiwe waoga kwani sisi tumechelewa katika hizi harakati naamini mtaendana na kasi ambayo tunataka ya kuitanga CUF kila mahali." alisema
Alisema atawapigania vijana wote ambao watashiriki katika nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya mitaa, vijiji, kata, wilaya, jimbo, mkoa na taifa ili kuendeleza chama chao.
Bobal aliwapa tahadhari vijana hao kuwa siasa si jambo la lelemama wanahitajika kujituma ili kuweza kufikia mafanikio kwani yeye mwenyewe amepitia changamoto nyingi hadi kufikia hapo alipo.
Mbunge huyo alisema historia yake alikuwa mwalimu wa Sekondari ambapo alipotangaza kujihusisha na siasa alipata changamoto kutoka kwa walimu wenzake ila leo amefanikiwab kuwa mbunge na kutumikia wananchi wa Mchinga.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mbunge wa Kilwa Kusini Seleman Bungara maarufu Bwege CUF, aliwataka vijana hao kujikita katika kutetea wanyonge kwani ndio njia ambayo itawasaidia kuchaguliwa na wananchi.
"Mimi nilifanikiwa kushinda ubunge kwa sababu nilikuwa natetea watu wanyonge nilipambana na watu matajiri lakini niliwashinda kwa sababu wananchi waliangalia mtu sahihi na si fedha," alisema.
Mbunge wa Liwale Zubeir Kuchauka CUF, alisema siasa ndio kila kitu katika maisha hivyo ni vigumu kutenganisha siasa na wananchi.
Kuchauka aliwataka vijana hao kuwa wavumilivu katika kupigania maslahi ya nchi kwa kuweka uzalendo mbele na haki.
Mwenyekiti wa Juvicuf UDSM, Jidawi Chande, alisema, tawi hilo kwa sasa lina vijana wanachama wa CUF zaidi ya 100.
Alisema changamoto walizonazo ni ukosefu wa ofisi hivyo kuwaomba wabunge hao kuwasaidia kupata ofisi ili waweze kufanya kazi cha chama kwa uhuru.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni