MTANZANIA AISHANGAZA DUNIA...WENGI HAWAKUAMINI
Mtanzania Adamu Gharibu Ali akisoma Qur'an huko Misri |
Mtanzania Adamu Gharibu Ali jana
alishangaza dunia katika fainali za mashindano ya Quran yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Azhari cha hapa Misri, kwa kuibuka
mshindi wa kwanza huku akiyabwaga mbali mataifa mengine kama vile Indonesia,
Nigeria na wenyeji wamisri waliyokuwa wakipewa nafasi kubwa ya ushindi,
mashindano hayo yalifanyika jana 30//6/2016 katika msikiti mkongwe na wa
kihistoria wa Al-Azhar uliyopo Hussein Darrasa.
Mashindano yamedhaminiwa na
Al-Imamu Akbar Sheikh Azahar Dr. Ahmad Twaibu, na yalikuwa yanamtafuta mtu
mwenye sauti mzuri zaidi ya kusomea Quran (اصوات Øسنة), mashindano yalianza
kabla ya ramadhani kwa njia ya mchujo washiriki zaidi ya 250 walijitokeza
katika mataifa 92 kwa hatua ya awali ya mchujo, na mpaka jana wanakwenda
fainali kulikuwa na makundi matatu ya washiriki 5 kila kundi na kulazimika
kwenda mchujo mara 4, na kubakia watu waliyompa ushindi Adamu Gharibu.
Kipaji cha Adamu Gharibu cha
sauti ya kusomea Quran kiligundulika toka akiwa mdogo lakini mpaka sasa amekosa
wa dhamini wa kumuendeleza, kati ya mwaka 2007 mpaka 2008 Adamu akiwa na umri
mdogo aliwai kuswalisha swala ya tarehewe Msikiti wa Omar bin khattab uliyopo
Jangwani DaresSalaam.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni