TAARIFA MUHIMU KUTOKA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU,SOMA HAPO KUJUA
Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu ilitoa notisi ya siku 60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo
yao.
Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri
kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho. Baada ya
kipindi hicho kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia
kimekwisha.
Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu
wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya
wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.
Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao
hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao. Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha
kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa
mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.
Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza
kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye
ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la
kutangaza majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:
A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka
usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.
Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu