Zinazobamba

JESHI LA POLISI MKOA WA DAR ES SALAAM LAINGIZA SH.MILIONI 198 KATIKA ZOEZI LA KUHAKIKI SILAHA 14107

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Sirro, akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana alipokuwa akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na mchakato wa uhakiki wa silaha.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Sirro, akiwaonesha waandishi wa habari bunduki aina ya gobore walioikamata kabla ya kutumika kwa ujambazi wakati akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya uharifu pamoja na mchakato wa uhakiki wa silaha mkoani humo leo mchana.
 Kamanda Sirro akionesha simu walizokutwa nazo watu wanaodaiwa vinara wa kupora simu kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali ya jijini.

 Wapiga picha za vituo mbalimbali vya televisheni wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.


Na Dotto Mwaibale

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa 
kuliingia mapato taifa ya sh.milioni 198 kutokana na zoezi la uhakiki wa silaha lililofanyika mapema mwaka huu.

Jeshi hilo limefanikiwa kuhakiki jumla ya silaha 14,107 kwa kipindi cha kuanzia Machi Mosi hadi Juni 30 mwaka huu, vile vile Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa sugu 1,065.

Hayo yameelezwa leo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro wakati akitoa taarifa za matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na zoezi la kuhakiki wa silaha hizo.

Alisema zoezi la uhakiki wa silaha lilihusisha mikoa ya kipolisi ya Temeke, Ilala na Kinondoni.

"Idadi ya watu waliojitokeza kuhakiki silaha kwa mikoa yote ni 11,602, na silaha zilizohakikiwa ni pistol 5,073, shotgun 4,707 na rifle 2,974," alisema.

Kamishna Sirro alisema dosari ndogo ndogo zilizojitokeza katika zoezi hilo ni kama vile wamiliki wa silaha kuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 70, na wengine kumili silaha za marehemu kinyume na taratibu.

"Hawa kwa kweli hatukuwaruhusu waendelee kumiliki hizo silaha, hivyo tulibaki nazo na wale walioshindwa kuzilipia silaha zao kwa muda mrefu pia tulibaki nazo," alisema.

Kamishna Sirro alisema kutokana na sababu hizo jumla ya silaha 66 walibaki nazo (kusalimishwa), ikiwa ni shotgun 36, rifle 10 na pistol 20.

Katika operesheni maalumu iliyowezesha kukumata watuhumiwa sugu 1,065, Kamishna Sirro alisema watuhumiwa hawo walikatwa kwa makosa mbali mbali yakiwemo ya makosa ya unyang'anyi wa kutumia nguvu.

"katika hawa tumefakiwa kuwakamata watengenezaji wa pombe haramu ya gongo wakiwa na lita 952 pamoja na mitambo mitatu, vile vile kuna wavutaji wa bangi na puli zao 277.

"Matukio mengine ni pamoja na kukamatwa kwa kete 210, misokoto 144, pamoja na wacheza kamari," alisema.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu  kwa makosa ya uporaji  wa simu katika maeneo mbali mbali ya kinondoni, mtuhumiwa wa kwanza ni Richard Augustino 18 aliyekamatwa Julai 11 mwaka huu maeneo ya Coco Beach akiwa na sumsung yenye thamani ya sh. 500,000.

"Wengine ni Abdalah Chande 36 aliyekematwa Julai 11 mwaka huu maeneo ya Magomeni Mapipa akiwa na simu 11 za wizi, na Abdalah Saidi 22 ambaye alikamatwa maeneo ya Mapipa julai 14 mwaka huu akiwa na pikipiki aina ya boxer ambayo ilikuwa ikitumika katika matukio ya ukuporaji simu," alisema.