CHUO KIKUU CHA MLIMANI CHAJIZATITI KUTOA ELIMU KWA AJILI TEKNOHAMA KWENYE UPANDE WA BIASHARA,SOMA HAPO KUJUA
WAKATI sekta ya Teknolojia ikiwa inakuwa kwa kasi
nchini,Chuo Kikuu cha Mlimani katika shule yake kuu ya Biashara wameendelea
kutoa elimu maalum ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA)
kwa wanafunzi wanaosoma shule hiyo ili
iweze kuwajengeo uwezo mkubwa katika ushindani wa Ajira.Anaandika KAROLI
VINSENT endelea nayo.
Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wakuwapatia
vyeti wanafunzi 117 ambao waliohitimu kozi hiyo , Mkuu wa Shule hiyo ya
Biashara,Dk Ulingeta Mbamba amesema pogramu hiyo itawasaidia watu wengi kuwa
wajuzi katika masuala ya biashara kwa upande wa sayansi.
Amesema njia ya kutoa elimu hiyo ni kuwasaidia
wanafunzi katika mfumo wa ajira jambo analodai litaweza kuinua sekta mbali
mbali za biashara.
“Hii pogramu tangu taanza mwaka jana teayri tumetoa
wahimu zaidi ya 200 lengo ni kuhakikisha watu wanakwenda na mabadiliko ya
sanyasi na teknolojia ambayo kwa sasa imekuwa inatumiwa katika kusimamia
biashara mbali mbali”amesema Dk Mbamba.
Kwa upande wake Mhadhili mkuu wa shule ya
Biashara,Dk Tumsifu Eli amesema kozi hiyo itawasaidia wahitimu kuweza kuzisimia
biashara kupitia mifumo mbali mbali.
Amesema Kozi itachangia kupunguza matumizi ya Hasara
ambayo yanaweza kutokea kwenye biashara.