Zinazobamba

ASKARI POLISI AUAWA MAZINGIRA YA KUTATANISHA,SOMA HAPO KUJUA


Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi Oysterbay ameuawa usiku wa kuamkia leo  kwa kupigwa risasi akiwa kazini eneo la Sayansi Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku huu na chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.

“Tukipata chanzo itakuwa tayari upelelezi wetu umetimia, hivyo kwa sasa tunalifanyia kazi ili kubaini wahusika wa mauaji hayo,” amesema Fuime.