CHADEMA YAKUTANA KWA DHARULA,YAJIPANGA KIMIKAKATI MIKUBWA,SOMA HAPO KUJUA
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), itakutana kwa dharura, jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa
Chama Taifa, Freeman Mbowe, ambapo pamoja na masuala mengine, itapokea taarifa
na kujadili hali ya siasa nchini.
Katika siku za hivi karibuni, taifa limekuwa
likipitia katika majaribu makubwa, ikiwa ni pamoja na uvunjifu mkubwa wa sheria
na taratibu za kuongoza nchi unaofanywa waziwazi na mamlaka za juu/viongozi
waandamizi wa nchi kupitia kauli na matendo mbalimbali kiasi cha kuwashtua
Watanzania ambao wangependa kuona nchi yao ikiendeshwa katika misingi ya
uwajibikaji wa kisheria na demokrasia.
Katika kikao hicho cha siku mbili, Julai 23-24,
mwaka huu, Kamati Kuu pia itapokea taarifa na kujadili kabla ya kufanya maamuzi
kuhusu mipango mbalimbali inayoendelea ya kukipanga chama ili kiendelee kufanya
shughuli zake kwa ufanisi hususani kinapokwenda kuimarisha misingi kuanzia
ngazi ya kitongoji nchi nzima, kupitia usimamizi wa kanda 10 za chama.
Imetolewa Ijumaa, Julai 22, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA