SINEMA YA POLISI NA WABUNGE WA CHADEMA YAANZA TENA,WABUNGE HAWA WASHIKILIWA,SOMA HAPO KUJUA
Jeshi la polisi mkoani Arusha, limewaita kwa
mahojiano, mbunge wa Karatu,Wilbroad Qambalo, mbunge wa viti maalumu Mkoa wa
Arusha, Cecilia Paresso na Mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu,Jubilate Mnyenye
kutokana na kupuuza agizo la kutofanya mikutano ya hadhara katika jimbo hilo.
Mwingine ambaye ametakiwa kwenda kuripoti polisi ni
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Lazaro Bajuta.
Wakizungumza jana baada ya kukabidhiwa barua za wito
wa polisi, Qambalo na Paresso walisema wamestuka kutakiwa kuripoti ofisi ofisi
ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha jumatano.
Parreso alisema,walipokea barua jana saa sita mchana
na kutakiwa kuripoti kwa RCO, saa nane lakini wakampigia na kumweleza
wana ratiba nyingine tayari waende jumatano na akakubali.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkombo
alipotakiwa kuelezea agizo hilo alisema yupo likizo