MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AJA MPANGO KABAMBE WA KUMALIZA TATIZO LA AJIRA,SOMA HAPO KUJUA
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi amesema amejidhatiti katika kuhakikisha anamaliza tatizo la ukosefu wa ajira katika wilaya hiyo baada ya kuanzisha mpango wa kuweza kutatua tatizo la ajira hususani kwa vijana.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Akizungumza na watendaji wa kata,wenyekiti wa serikali za mitaa pamoja wajumbe wa maeneo,katika manispaa hiyo,Hapi amesema amekusudia kumaliza changomoto ya ajira kwa vijana kwa lengo la kumaliza tatizo la uharifu analodai linachangiwa na ukosefu wa ajira.
Amesema kwa sasa ameandaa mpango ambao watendaji hao wa kata,vijiji wanatakiwa kwenda Nyumba hadi nyumba kuchukua orodha ya majina ya vijana ambao hawana ajira ili aweze kuwaunganisha na wajasiriamali,makampuni pamoja na wafanya biashara wakubwa ili waweze kuwasaidia na tatizo la ajira.
Amewataka wananchi wote wa wilaya ya kinondoni kujitokeza kuandika majina siku tarehe 1 hadi tarehe 7 ya mwezi wa 8 mwaka huu kujiandikisha majina hayo.
Hapi amefafanua kuwa mara baada ya kumalika kuchukuliwa majina hayo ambapo siku ya tarehe 15 ya mwenzi wa 8,wananchi hao waliandishwa majiana hayo watakutanishwa katika viwanja vya Posta Kijitonyama ambap siku hiyo wataunganishwa na wadau hao wa maendeleo.
Aidha, Hapi amewasahii watendaji hao pamoja wajumbe wa kata kuweka ushirikiano katika mpango huo ili kuhakikisha wanaweza kumaliza tatizo la ajira.