Zinazobamba

PPRA YABAINI MADUDU TAASISI ZA SERIKALI,TAASISI ZAIDI 300 ZAIGOMEA,SOMA HAPO KUJUA



IMG_0086


pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti Manunuzi ya Serikali (PPRA) Dk  Marterm Lubanga akizungumza na waandishi wa habari

NA KAROLI VINSENT
MAMLAKA ya udhibiti  Manunizi ya Serikali(PPRA) imesema taasisi145 tu kati taasisi 506 ndio zimewasilisha mpango wa manunuzi kwa mwaka (GNP)  hali hiyo imepelekea serikali kupoteza mamilioni ya fedha na huku ikichangia kuwepo  vitendo vya rushwa pamoja na kutokea ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ya umma.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya (PPRA) Marterm Lubanga wakati wa mkutano na waandishi wa habari,amesema kitendo cha Taasisi hizo kushindwa kuwasilisha taarifa hizo,wanakuwa wamekiuka sheria ya Manunuzi ya Umma namba ya 7 ya mwaka 2011 ambayo inawataka kuwasilisha  kwenye Mamlaka hiyo mipango yao ya manunuzi ya mwaka kabla ya mwaka wa fedha mwengine haujaanza.

Dk Lubanga amesema licha ya Mamlaka hiyo kufunya juhudi za kuwakumbusha taasisi hizo kuhusu jukumu lao la kuwasilisha taarifa hizo kama sheria inavyotaka lakini bado taasisi hizo zimeshindwa kutoa ushirikiano.

Amesema PPRA imebaini kuwepo kwa taasisi ambazo zimekuwa zikichapisha  GPN zao kwenye Magazeti bila ya kuwasilisha katika mamlaka hiyo jambo ambalo ni kinyume na sheria.


“Sheria ambayo  inawataka  kuchapisha kwenye jarida la manunuzi na tovuti ya PPRA pekee,mwezi mmoja kabla ya kuanza michakato ya zabuni zilioanishwa kwenye GNP ya mwaka wa fedha husika”amesema Dk Lubanga.

Hata hivyo,Dk Shilima amesema kitendo cha taasisi hizo kutowasilisha Mpango wa manunuzi wa mwaka umeleta athari kubwa kwa serikali.

Ametaja athari hizo kuwa ni kutokuwa na uwazi katika manunuzi makubwa ambayo yanatumia fedha nyingi za umma huku akitolea mfano  miradi mingi yenye thamani kubwa ambayo PPRA imeifanyia uchunguzi na kubaini kuwepo na upungufu mkubwa.
Amesema, Taarifa ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali  ya mwaka 2014/2015 ilibainishwa kwamba manunuzi shilingi bilioni 8.5  ambayo hayakuwa yamejumuishwa kwenye mapango wa manunuzi  jambo linalopelkeea kuwepo kwa ufufishaji wa jukumu la  PPRA katika usimamizi na udhibiti.
Aidha,Dk Lubanga amesema  kutokana na taasisi hizo kushindwa kuwasilisha GNP zao kwa mwaka uliopita wa fedha uliopita 2015/2016 ,PPRA inazitaka Mamlaka nyingine ya serikali kuchukua hatua  dhidi  ya mafiasa masauli wa taasisi hizo kwa kushindwa kusimamia  utekelezaji wa sheria hizo,