NCHI WANACHAMA WA EAC WAASWA KUUNGA MKONO MSWADA WA KIJINSIA, WANAHARAKATI WASEMA UKIPITA UTALETA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA MAENDELEO
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameaswa kuunga mkono mswada wa sheria ya usawa wa kijinsia na maendeleo kwani kufanya hivyo kutasaidia kukuza usawa wa kijinsia katika nchi hizo na hivyo kuweza kuinua uchumi wa watu wake
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki lazima ikubali kuondokana na mfumo dume kwa kuunga mkono mswada huo ambao umelenga kukuza usawa wa kijinsia katika Nchi Tano za Afrika Mashariki katika nyanja za kiuchumi,kisiasa,kijamii na kiutamaduni kwa manufaa ya wanawake na wanaume
"Lengo kuu la mswada wa sheria ya usawa
wa kijinsia na maendeleo wa jumuiya ya Afrika mashariki ni kukuza usawa wa
kijinsia katika nchi tano wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki katika
Nyanja za kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni kwa manufaa ya wanawake na
wanaume kwa kuziunganisha katika andiko moja la kisheria njia mbalimbali za
kudai haki za binadamu ambazo nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki
wameziridhia katika ngazi ya bara na kimataifa. (Azimio la Beijing, CEDAW, itifaki ya mkataba wa Afrika kuhusu haki za
binadamu na watu ikilenga haki za wanawake Afrika, na malengo ya maendeleo
endelevu ya kidunia hususani lengo la 1 kuhusu umasikini, lengo la 5 kuhusu
usawa wa kijinsia.)" Alisema
Kampeni hii
ilichagizwa na kampeni kama hii katika jumuiya ya nchi za kusini mwa bara la
Afrika (SADC) iliyofanywa na mashirika ya wanawake kusini mwa Afrika
kushinikiza uwepo wa tamko la SADC kuhusu jinsia ambalo baadae lilibadilika na
sasa linajulikana kama itifaki ya jinsia ya SADC.
Kwanini mswada wa sheria ya jinsia na
maendeleo wa EAC?
Nchi wanachama wa EAC
zimesaini na kuridhia mikataba na matamko mbalimbali za kikanda na kimataifa yanazohusiana
na usawa wa kijinsia na haki za wanawake na zina sheria na sera za kitaifa
kuhusu usawa wa kijinsia. Hata hivyo, njia hizi ama hazijatiliwa mkazo au
hazitatekelezwa ipasavyo ili kulinda haki za wanawake.
Hali hii imewafanya wanawake
waendelee kuwa waathirika wa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na
imezidisha kiwango cha kutokuwepo kwa usawa katika utawala na shughuli za
kibiashara katika ngazi ya kanda, taifa na jamii.
Kwa mfano, wanawake kwenye nchi kama
Kenya, Tanzania na Uganda bado wanakumbana na ukeketaji japokuwa kuna sheria
zinazokataza jambo hilo. Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF kuhusu ukeketaji mwaka
2013, 27% ya wasichana nchini Kenya wanafanyiwa ukeketaji, 88 nchini Sudan,
wakati Tanzania imeongezeka kutoka 28.4% mpaka 31.7% na 1% nchini Uganda.
Kuhusu
suala la afya, afya ya uzazi, hali siyo ya kuridhisha kwa nchi zote. Kwa mujibu
wa Shirika la Afya duniani (WHO), viwango vya vifo vitokanavyo na uzazi (kwa
wastani wa vizazi hai 100,000) kwa nchi wanachama wa EAC ni kama ifuatavyo:
Burundi vifo 740, Kenya 400, Uganda 360, Tanzania 410 na Rwanda 320. Viwango
hivi vi vya juu sana nab ado nchi husika hazitengi 15% ya bajeti zao kwa ajili
ya afya kama ilivyokubaliwa kwenye tamko la Abuja lililozipa nguvu nchi za
kiafrika kutenga asilimia hiyo.
Hii ni mifano michache tu ya hali
kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia kwenye nchi wanachama wa EAC. Nchi wanachama
wa EAC wanawajibika kutekeleza njia, sera, sheria, kutenga fedha za kutosha na
kuchukua hatua madhubuti kuweza kukabiliana na hali ya kutokuwepo kwa usawa wa
kijinsia na kusimamia haki za wanawake na kuondoa vikwazo vinavyokwamisha
maendeleo ya wanawake.
Tuatarajia kwamba
mara baada ya mswada kuridhiwa na kuwa sheria utazioanisha sheria za nchi
wanachama wa EAC na viwango vya kikanda na vya kimataifa vya ulinzi na ukuzaji
wa haki za kijinsia na za binadamu, itaendeleza hali ya usawa wa kijinsia na
kutokubaguana katika nafasi za maamuzi na uongozi na biashara kwa lengo la
kuimarisha fungamano la kikanda na maendeleo endelevu ya jumuiya.
Halikadhalika sheria itakuza ushiriki sawa wa wanawake na
wanaume ktika biashara ya kikanda kwa kuanzisha sera za kusaidia na mifumo ya
biashara kubwa ambayo inatambua na kuheshimu jinsia zote.
Ndugu
wana habari,
Awamu hii siyo tu kwamba tunasukuma
kupitishwa kwa sheria kwenye karatasi ila tuna nia thabiti ya kupima mwelekeo
wa serikali zetu na utendaji wao katika kutekeleza majukumu yo kuhusu usawa wa
kjinsia na maendeleo.
Kwa mara ya kwanza Afrika mashariki tunakwenda
kuanzisha kipimo cha hali ya usawa wa kijinsia ndani ya EAC sawa na kile cha
nchi za SADC. Taarifa ya hali ya jinsia ndani ya EAC itakayojumuisha kiashiria
cha mtizamo wa wananchi itatoka mwezi Oktoba mwaka huu na itahuishwa kila
mwaka.
Kwa sasa hakuna utaratibu wa
kisheria unaotoa taarifa za kimamlaka au takwimu zinazoweza kutumiwa kuziwajibisha
nchi wanachama wa EAC kuhusu majukumu yao yahusuyo masuala ya jinsia. Japokuwa
takwimu zisizo rasmi zinakusanywa kuhusu mambo tofauti kwa nyakati tofauti,
ushahidi katika tafiti hizo mara nyingine hukosa uthibitisho wa kisayansi au
tamko la wazi kuhusu matokeo yanayoambatana na kukosekana kwa uwajibikaji wa
pamoja miongoni mwa nchi wanachama.
Kipimo cha hali ya jinsia ndani ya EAC kitakuwa nyenzo
kuu itakayofuatilia na kutoa taarifa juu ya haki za wanawake na usawa wa
kijinsia ambazo zitakuwa rahisi kueleweka na kusambazwa.
Kipimo cha hali ya jinsia
kinatarajiwa kutizama masuala ya usawa wa kijinsia na kufanya ufuatiliaji mara
kwa mara. Taarifa ya ufuatiliajiitakuwa muhimu kwa wafanya maamuzi kuona ni kawa
namna gani nchi zao zimeweza kutekeleza majukumu yao kuhusua masuala ya jinsia.
Kuwepo kwa kipimo cha hali ya jinsia ni njia muhimu
siyo tu ya kuboresha ushirikiano wa wananchi katika masuala ya utawala kwa
kuwapatia taarifa muhimu bali ni njia pia ya kuziwajibisha serikali katika
utekelezaji wa majukumu yao yahusuyo masuala ya jinsia.
Sheria ya
usawa wa jinsia na maendeleo ya Afrika mashariki imechelewa sana! Tunalisihi bunge
la Afrika mashariki (EALA) kuharakisha majadiliano ya wazi ya wananchi kuhusu
mswada na hatua ya kuupitisha kuwa sheria.
Tunazisihi
nchi wanachama wa EAC kuunga mkono mswada wa usawa wa kijinsia na maendeleo wa
jumuiya ya Afrika mashariki!
Asasi ya kusaidia na kuhamasisha maendeleo ya wanawake katika ukanda wa Afrika mashariki (EASSI) yenye miaka 20 sasa, ni asasi ya kiraia ya kikanda iliyoanzishwa mwaka 1996. EASSI ina dhima ya kuwezesha ufuatiliaji wa utekelezaji wa mpango kazi wa Beijing (Beijing Platforms for Action [BPFAs]) ambacho ni chombo cha Mkutano wa nne wa wanawake uliofanyika mjini Beijing nchini China mwaka 1995 na mkutano wan ne wa wanawake Afrika uliofanyika Dakar, Senegal. Asasi hii, ambayo imesajiliwa nchini Uganda kama asasi ya kiraia, inafanya kazi na asasi nyingine za kitaifa katika nchi nne zikiwamo Burundi, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Tanzania na Uganda.
Asasi ya kusaidia na kuhamasisha maendeleo ya wanawake katika ukanda wa Afrika mashariki (EASSI) yenye miaka 20 sasa, ni asasi ya kiraia ya kikanda iliyoanzishwa mwaka 1996. EASSI ina dhima ya kuwezesha ufuatiliaji wa utekelezaji wa mpango kazi wa Beijing (Beijing Platforms for Action [BPFAs]) ambacho ni chombo cha Mkutano wa nne wa wanawake uliofanyika mjini Beijing nchini China mwaka 1995 na mkutano wan ne wa wanawake Afrika uliofanyika Dakar, Senegal. Asasi hii, ambayo imesajiliwa nchini Uganda kama asasi ya kiraia, inafanya kazi na asasi nyingine za kitaifa katika nchi nne zikiwamo Burundi, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Tanzania na Uganda.
Kuanzia mwaka
2008, EASSI kwa kushirikiana na mashirika yanayopigania haki za wanawake
ikiwemo TGNP Mtandao (Tanzania) katika nchi tano washirika imekuwa ikifanya
kampeni kuhusu upatikanaji wa itifaki ya usawa wa kijinsia ya Afrika mashariki.
Itifaki hii ilibadilika baadae na kuwa mswada ambao uliwasilishwa kwenye bunge
la JUMUIYA YA Afrika mashariki kama mswada binafsi na hivyo kuwa tayari
kusikilizwa na umma katika nchi tano wanachama.