UKUTA YA CHADEMA YAMTISHA MSAJILI WA VYAMA,AIBUKA NA KULALAMA NA HILI,SOMA HAPO KUJUA
JAJI Francis Mutungi, Msajili wa vyama vya siasa
hapa nchini amekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu
mikutano ya hadhara na maandamano yanayotarajia kuanza 1 Septemba mwaka huu, anaandika Pendo Omary.
Siku ya Jana, Freema Mbowe Mwenyekiti wa Chadema taifa
alitangaza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi kwa dharura huku
kufanyika kwa mikutano ya hadhara na maandamano kote nchini kuanzia 1 Septemba
ikiwa ni miongoni mwa maazimio hayo.
Katika
tamko hilo lililotolewa na Mbowe, aliwataka viongozi wa Chadema katika ngazi
zote hapa nchini, wabunge na madiwani kufanya maandalizi ya mikutano na
maandamano huku pia akitangaza kuanzishwa kwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania
(UKUTA).
Hata
hivyo, Jaji Mtungi mapema hii leo amevieleza vyombo vya habari kuwa, “tamko la
Chadema limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, linaloudhi na lenye kuhamasisha
uvunjifu wa amani.”
Huku
akitahadharisha kuwa, Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 katika
kifungu cha 9 (2) (c) inakataza chama chochote cha siasa hapa nchini kutumia na
kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake
kisiasa.
“Si
hivyo tu, bali pia kifungu cha 9 (2) (f) kinakataza chama cha siasa kuruhusu
viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambao
unaweza kusababisha kutokea kwa uvunjifu wa amani,” amesema Jaji Mutungi.
Mvutano
baina ya Chadema na Jeshi la Polisi juu ya kufanyika kwa mikutano ya hadhara
umekuwa ukiendelea kwa muda sasa, kufuatia Jeshi hilo kutoa tangazo la kuzuia
mikutano ya hadhara Juni mwaka huu kwa madai ya kuwepo kwa viashiria vya
uvunjifu wa amani