Zinazobamba

MANISPAA YA KINONDONI YATUMBUA JIPU KWA WATUMISHI WAKE,SOMA HAPO KUJUA


Pichani ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Boniface Jacob


BARAZA la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni limewafukuza kazi watumishi wanne katika idara ya afya baada ya kudhibitika kuwa na makosa ya utoro kazini na Rushwa.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Mbali na hao pia Baraza hilo limewashusha vyeo  na madaraja wahandisi 2 huku mhandisi 1  na mwengine  mtumishi wa idara ya fedha na Biashara ambao wao wamepewa adhabu ya onyo kali baada ya kufanya makosa kwenye majukumu yao.

Akisoma Hukumu hiyo leo Jijini Dar es Salaam,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Boniface Jacob amesema hukumu hiyo imetolea na Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo katika mkutano wake maaulumu wa mashauri ya nidhamu uliofanyika hivi 
karibuni,ambapo mkutano huo pamoja na mambo mengine ilikuwa ikijadili na kutoa maamuzi ya nidhamu.

Amesema katika mkutano huo watumishi 18 walifunguliwa mashauri ya kinidhamu  ambapo kati yao  watumishi  9 ni wa idara ya  Uhandisi ,watumishi 8 ni wa idara ya afya huku mtumishi mmoja ni wa idara ya fedha na Biashara.

Amesema Baraza hilo limewachukulia hatua Wahandisi hao baada ya kubainika  kushindwa kutumia taaruma zao  vizuri katika kuisimamia katika ujenzi wa Barabara ya Biafra ambapo barabara hiyo imegundulika kuwepo kwa makosa.

Jacob ambaye ni Diwani wa Kata ya Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema amesema Baraza lake katika kuwachukulia hatua watendaji hao limezingatia hatua zote ikiwemo kufanyika kwa uchunguzi wa awali kuhusu tuhuma zao pamoja na kufungua mashtaka kuhusu tuhuma hizo.


Amesema Watumishi hao waliwasilisha utetezi wao katika tuhuma zao ndani ya siku 14 baada ya kusimamishwa kazi ikiwemo  kuwaundia uchunguzi.

Katika hatua nyengine,Baraza hilo lilijadili kwa kina na kuridhia kutoa kibali cha kuwapandisha vyeo watumishi 372,kubadili vyeo watumishi 9 na kuwadhibitisha kazini watumishi 206 ambao wamemaliza vipindi vyao vya majaribio  baada kuonekana wanafaa kufanya kazi katika utumishi wa umma.