MEYA WA UKAWA KINONDONI APANIA KUIPANDISHA TIMU YA MPIRA KINONDONI LIGI KUU,SOMA KUJUA
Meya wa Ukawa Manispaa ya Kinondoni,Bonifacce Jacob |
MEYA wa Manispaa ya Kinondoni,Bonifacce Jacob amesema
amepania kuifanikiwa timu ya Mpira wa
Miguu ya Manispaa hiyo KNFC inafaniki
kuingia ligu kuu ya Tanzania bara katika msimu ujao.Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Jacob ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam
wakati alipozungumza na wadau mbali mbali wa mpira wa Miguu katika Manispaa
hiyo ambao aliitisha mkutano na wadau hao ili kujadili njia ya kuisadia timu
hiyo ambayo ipo kwenye ligi daraha ya kwanza.
Amesema kwa sasa Manispaa hiyo katika Bajeti yake wametenga fedha ambazo zimepelekwa kwa timu hiyo ili iweze
kuisadia timu hiyo kupata matokea mazuri ambayo yataisadia mpaka kuingia ligi
kuu.
Amesema licha ya kutenga fedha kwenye timu hiyo
katika msimu ujao lakini ilifanikiwa kushika nafasi ya pili katika ligi ya
kwanza nyuma ya timu ya Afrika Lyoni ambayo ilifanikiwa kuingia ligi kuu ,jambo
lilimshangaza kwa kile anachosema timu ya Kinondoni imewekea mazingia yote ya
rafiki kwanini ilishindwa kuingia ligi kuu.
Aidha,Jacob amewataka wadau kujitolea kwa hali na
mali na kutoa tofauti zozote
zilizojitokeza ili kuisadia timu hiyo kufanikisha kushiriki kwenye ligi kuu
msimu ujao.
Kwa upande wake wadau mbali mbali
waliojitokeza,waliiomba manispaa hiyo kuishirikisha Chama cha mpira wa Miguu
wilayani humo,(KIFA) katika safari zote za mechi za timu hizo itakazo cheza,jambo
wanalodai litaweza kuiasadia timu hiyo kufanya vizuri.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni