SUMAYE AWAANGUKIA WATANZANIA,NAYE MEYA WA MANISPAA YA ILALA NA MKURUGENZI WAKE WATOA NEO,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Waziri mkuu mstaafu,Fredrick Sumaye picha na Maktaba |
WAZIRI mkuu mstaafu,Fredrick Sumaye amewaomba
watanzania bila kujali tofauti za dini,kuliombea taifa kwakuwa linapitia
kipindi kigumu.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Sumaye alitoa kauli hiyo jana jioni wakati wa mlo wa
Futari ilioyoandaliwa na Meya wa Manispaa ya Ilala,Chalres Kuyeko pamoja na
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Isaya Mungurumi kwa ajili ya Dini ya Kiislam pamoja
na Dini zengine.
Amesema kwa sasa taifa linaitaji maombi ili liweze
kutoka hapa lilipo ambao kwa mujibu wa sumaye anasema kwa sasa taifa linapitia
wakati mgumu ambao unatokana na tatizo
la ombwe la uongozi.
Amesema Jukumu jukumu la kulitoa Taifa kwenye hali
hiyo ni kila mtanzania mwenye mapenzi
mema anawajibu wa kujibidisha katika kusali ili taifa lisonge mbele.
Amebanisha kuwa dua za watanzania kwa taifa kutawapa
watawala nguvu na kuweza kufanya yale ambayo Mungu anayataka katika kuwatumikia
watanzania ili waweze kuishi kwa amani.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Ilala,Chalres
Kuyeko amewataka wakazi wa manispaa hiyo kijibidisha katika kulipa kodi ili
manispaa hiyo iweze kufikia malengo ya maendeleo wanayoyawataka.
Amesema njia pekee itakayoweza manispaahiyo kufikia
malengo ambayo kila mwana ilala anayoyataka yatafikia endapo wanachi hao
watajiibidisha katika kulipa kodi.
Naye,Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Mungurumi naye
amewashihi wakati wa manispaa hiyo kuzidisha upendo na kufanya mambo ya
kumpendeza mungu na kuacha kufanya mambo ya maomvu ambayo anadai yatamchukiza
mwenyezi Mungu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni