SHEIKH WA MKOA: TUNAPASWA KUWAUNGA MKONO WAPALESTINA
Wanasemina wakifuatilia kwa makini semina hiyo. |
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Daresalaam, Alhadi Mussa Salum ameitaka jamii husani wale wote wanaopenda Amani duniani kuhakikisha wanapinga vikali vitendo vya dhulma vinavyoendelea Nchini Palestina.
Alhadi Mussa aliyasema hayo katika
semina Maalum iliyowakutanisha wataalamu mbalimbali yenye lengo la kujadili
hali halisi ya nchini Pakstani, Mkutano uliofanyika katika viwanja vya Karimjee
Jijini Daresalaam.
Amesema vitendo vinavyofanywa na
Wazayni kwa wazawa wa Wapalestina havikubaliki na binadamu yeyote anayependa Amani,
na kwamba Waislamu wa Tanzania wangependa kuona hali ya Palestina inatengemaa
na wakazi wake wanaishi kwa Amani, upendo na furaha kama nchi zingine.
“Suala la maisha ya wazawa wa
Palestina ni suala la kila mmoja wetu duniani, tunapaswa kupaza sauti kuhakikisha hatua ya kuwanusuru
wapalestina inafikiwa kwa haraka na hivyo kuwaondolea adha kubwa wanayoipata
kila leo”Alisema Sheikh Alhadi Mussa.
Katika hatua
Nyingine Sheikh Alhadi Mussa amewataka Waislamu kudumisha matendo mema
waliyoyafanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani katika miezi mengine yote kwani
Mungu wa Ramadhani bado anaishi na anakuona katika miezi mengine yote.
Alisema Waislamu wanapaswa kufahamu
kuwa kuisha kwa Mwezi wa Ramadhani haina maana kuwa ndiyo mwanzo wa kuanza
maovu, badala yake mwezi huo uwabadilishe watu tabia zao na waweze kuwa watu
wapya kuanzia matendo yao n ahata kuishi kwao.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni