LOWASSA AMPASHA MAGUFULI.ASEMA NJIA NYEUPE 2020,AWAONEA HURUMA WATANZANIA KWA MATESO WANAYOYAPATA,SOMA HAPO
EDWARD Lowassa, aliyekuwa Mgombea Urais kupitia
Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), amesema safari ya upinzani kushika
dola 2020 njia yake ni nyeupe, anaandika Faki Sosi.
Lowassa ambaye aligombea urais kupitia
chama hicho na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) amesema kuwa, serikali ya Rais John Magufuli inarahisisha upinzani
kushika dola kwenye uchaguzi mkuu ujao kutokana na kushindwa kuwatumikia
wananchi.
Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kikao
cha Kamati Tendaji ya Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).
Lowassa amesema kuwa, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
inawanyima maisha ya raha na amani Watanzania kutokana na maisha kuwa magumu.
“Hakuna anayependa maisha haya, kwa namna yoyote
hakuna anayependa kushinda njaa. Maisha haya hakuna anayeyatamani.
“CCM inawaonjesha maisha magumu Watanzania, pesa
imekuwa ngumu kupatikana,” amesema Lowassa.
Amesema kuwa, ili Chadema kishinde 2020 ni lazima washirikiane na
kwamba, wasikubali kufitinishwa.
“Kuna watu maalum wameajiriwa na serikalai kwa ajili
ya kutugombanisha, watu hao ni maofisa usalama. Mfumo huu si wa hapa nchini tu,
hata huko nje huwa hivyo hivyo,” amesema Lowassa.
Pia Lowassa amekosoa uteuzi wa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi katika halmashauri mbalimbali nchi.
Amesema, uteuzi huo umefanywa kibaguzi na kuwa
haukuzingatia vijana kutoka katika vyama vingine ambavyo vina vijana wenye
uwezo na utashi wa uongozi.
“Serikali inasera ya kuongeza ajira kwa vijana, ni
kwanini wanabagua? kwanini nyinyi hamjasoma?” amewahoji vijana wa Bavicha.
Hata hivyo, amewapongeza vijana hao kwa kutii katazo
liliotolewa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa kutokana na dhamira
yao ya kutaka kuzuia mkutano wa CCM unaotarajia kufanyika mkoani Dodoma.
Lowassa amewaambia kuwa, hata yeye alipokuwa kijana
alishiriki katika kupinga mambo mbalimbali ambayo yangeweza kuathiri
maslahi ya nchi na kwamba, Mwl. Julias Nyerere aliwapongeza.
Lowassa amewasisitiza vijana hao kuwa na mshikamano
wa kujenga chama kuanzia ngazi za vjijini.
Hamis Mgeja, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Shinyanga amesema kuwa, nguvu ya mabadiliko imewashtua CCM na kwamba,
wamekuwa wakihangaika kutumbuana.
Amesema kuwa, serkaili imekuwa ikiteleza na kuogopa
kukoselewa na kuwa “wamekuwa wakiwafunga midomo wapinzani ili wanyamaze.”