MWANAMKE ALIYEPIGA PICHA ZA UTUPU AFUNGUKA NDOA YAKE YAVUNJIKA,SOMA HAPO KUJUA
Kuna picha zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii
zikimuonesha mwanamke akifanya mapenzi na mpenzi wake. Yote hayo yalitokea siku
chache tu baada ya mwanamke huyo kufunga ndoa na mwanaume mwingine jijini Dar
es Salaam.
Mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo alijipiga na
mpenzi wake zamani miaka saba iliyopita wakiwa chuoni na zimekuja kusambaa
ndani ya wiki baada ya kufunga ndoa. Anadai kuwa ni kisasi cha ex wake
aliyedhamiria kuivunja ndoa yake.
Akiongea kwenye Ripoti ya Siku ya kipindi cha Ubaoni
cha EFM kilichoruka Ijumaa iliyopita, mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo
zimedhamlilisha mno kiasi cha kuiharibu ndoa yake, kuwaumiza ndugu zake na
kuwakosea heshima wakwe zake na kwamba anajuta kupita kiasi.
“Ni kweli ni mimi ndiye niliyepiga hizo
picha lakini ni muda mrefu tangu kipindi nikiwa chuo, yaani hata huyo mtu
mwenyewe sijui yuko wapi sina mawasiliano naye tena, sikutegemea kiukweli,” anasema
mwanamke huyo.
“Ni kitu ambacho kinaniuma na
kimeniharibia mlolongo mzima wa maisha yangu, mpaka sasa hivi sielewi, mume
wangu hawezi kunielewa tena na yeye ndio nimemwekea kama nguzo, ndio kila kitu
kwasababu hata familia yangu hainielewi ,” ameongeza.
“Mpaka sasa hivi sijui nafanya nini.”
Kwa upande wa mume wake, alidai kuwa picha hizo
zimeuvunja moyo wake.
“Tulikuwa tumeshaenda kwenye honey moon
tumerudi, sikuamini macho yangu baada ya kuona hizo picha na huyu mwanamke,
rafiki zangu walikuwepo wengi sana, best man wangu pia ni vitu ambavyo
kuvizungumza mimi nashindwa, naanzia wapi, lakini mapenzi huwa yako hivyo,
inawezekana iko hivyo lakini sasa kama mazingira kama yale hata kama ukiwa ni
wewe lazima utaumia, familia yangu ntaiambia nini mimi, imenigharamia harusi
kubwa,” alisema mwanaume huyo.
Amedai kuwa haoni kama inawezekana tena kukaa chini
na mke wake huyo kwa kile kilichotokea.
“Nikae chini ili iweje?” alihoji kwa
jazba. “Imeniuma, imeniumiza sana hii kitu haki ya Mungu, hata kama miaka kumi
imepita kwanini imekuja kwenye harusi yangu, zawadi zimekuja kwaajili ya harusi
yetu kwanini aletewe picha za aina hiyo? Angeniambia before kwamba nilikuwa na
moja mbili, ningekuwa najua, lakini amenificha. Imenicost kwa kiasi kikubwa
sana, nitaiambiaje familia yangu kwa mfano? Nitasema nini.”
“Sitokuja kupenda tena mwanamke wa aina
yoyote ile, mpaka nakuja kuingia kaburini, I swear to God, imetosha kabisa.”
Wawili hao walifunga ndoa tarehe April 23 mwaka huu.
Kwa mujibu wa best man wa harusi hiyo, waliziona
picha hizo siku nne baada ya harusi wakati wanafungua zawadi walizopewa na
kuzikuta zikiwa kwenye bahasha na kusababisha vita kubwa kwenye familia yao.
Anadai kuwa rafiki yake hataki kusikia chochote
kuhusiana na kumsamehe mke wake na jitihada za ndugu kuwasuluhisha zimegonga
mwamba.
“Yaani hapo alipo nakuambia haelewi, mtu anayenisikiliza ni mimi tu, hasikilizi mtu yeyote. Huyo mwanamke ndio analia muda wote, jamaa haelewi,” amesema best man huyo aliyejitambulisha kwa jina la Geofrey Nicholas
“Yaani hapo alipo nakuambia haelewi, mtu anayenisikiliza ni mimi tu, hasikilizi mtu yeyote. Huyo mwanamke ndio analia muda wote, jamaa haelewi,” amesema best man huyo aliyejitambulisha kwa jina la Geofrey Nicholas